AHLUBAYT NDANI YA TAFSIRI ZA KISUNNI SEHEMU YAKWANZA
AHLUBAYT NDANI YA TAFSIRI ZA KISUNNI SEHEMU YAKWANZA
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2011
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
AHLUBAYT NDANI YA TAFSIRI ZA KISUNNI SEHEMU YAKWANZA
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Ahlu ‘l-Bayti Fi Tafasiri Ahli ‘s-Sunnah kilichoandikwa na Sheikh Nazri Hasan. Sisi tumekiita, Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni. Hii ni sehemu ya tatu inayochambua tafsiri za wanavyuoni wakubwa wa Kisunni – Ibn Kathir, Suyuti, Burusawi, Alusi na Qasimi. Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu!, Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja. Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi na misimamo ya wengine. Ni muhimu kufikiria kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba (Abu Batul) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.