Drawer trigger

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

Mtarjum :

HARUN PINGILI

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

AL-SAHIFATU AL-KAAMILATU AL-SAJJAADIYYATU

Tunamshukuru Allah (s.w.t) na baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na Ahlul Bayt (a.s) kwa kutujaalia kuweza kufanikia juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki "Sahifatul Kamillah Al-Sajadia". Kitabu kilochopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha Kiarabu, kiitwacho "As-Sahifatul Kamillah Al-Sajadia" kilichoandikwa na Imamu wa Nne Al-Imam Zainul Abdeen (a.s). Ndani ya Kitabu hiki Imam (a.s) ameelezea Du'a mbali mbali. Sababu iliyoifanya Mission yetu isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambayo zinatokana na maombi ya Maulamaa wengi katika Afrika Mashariki kututaka tukifanyie tarjuma kitabu hiki kiingie kwenye lugha ya Kiswahili. Tunamshukuru Shaikh Harun Pingili kwa kutukubalia ombi letu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja, na vile vile Bilal Muslim Mission of Scandinavia kutukubalia kukichapisha kitabu hiki. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tena kwani vitabu vyetu vya mwanzo vimependwa mno na wasomaji na hivyo kutupa ari ya kuchapisha hiki ulichonacho mkononi na kitakachofuatia Insha-Allah. Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika tarjuma na uchapishaji wa kitabu hiki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) awalipe malipo mema hapo Duniani na baadaye huko, Akhera.