Nchi na Uraia haki na Wajibu kwa Taifa
Nchi na Uraia haki na Wajibu kwa Taifa
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2013
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Nchi na Uraia haki na Wajibu kwa Taifa
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa mihadhara ya Sheikh Hassan Musa al-Saffar aliyokuwa akiitoa nyakati mbalimbali na sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuzungumzia mada mbalimbali kuhusiana na Uislamu, Waislamu na ubinadamu kwa ujumla.
Kama tunavyosema wakati wote kwamba Uislamu ni dini na mfumo kamili wa maisha; haukuacha lolote linalomhusu mwanadamu kimwili au kiroho na kuweka sheria ya kuyaendesha maisha hayo (kiroho na kimwili).
Katika kitabu hiki Sheikh anazungumzia suala la haki na wajibu wa raia katika taifa kwa mtazamo wa Kiislamu.
Sisi kama wachapishaji tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo ndani yake, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyomo humo.
Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya Al-Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu hususan wanaozungumza Kiswahili.