Drawer trigger

ABU HURAIRA

ABU HURAIRA

ABU HURAIRA

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2011

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

ABU HURAIRA

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Abu Huraira, kilichoandikwa na Sayyid Abdulhusain Sharafuddin al-Musawi. Kitabu hiki kinazungumzia maisha na wasifu wa sahaba machachari wa Mtukufu Mtume SAW na jinsi alivyoitumia nafasi hii pamoja na fursa alizozipata. Mwandishi wa kitabu hiki amefanya utafiti wa kina juu ya maisha ya sahaba huyu kwa sababu moja kubwa aliyoisema, ambayo ni umaarufu wake katika wingi wa hadithi alizosimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume SAW mbali ya kweli kwamba aliishi naye kwa muda mfupi sana ukilinganisha na masahaba wengine. Hii ndio sababu kubwa iliyomfanya mwandishi huyu afanye utafiti juu ya sahaba huyu ili kujua undani wake. Ni muhimu kumjua mtu kama huyu kwani aliyosimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume SAWni mengi sana yakiwemo ya ukweli na kusingizia, na ya kuongoza na kupotosha. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana , hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhan S. K. Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.