Drawer trigger

adhana_kwa_mtazamo_wa_qurani_na_sunna

adhana_kwa_mtazamo_wa_qurani_na_sunna

adhana_kwa_mtazamo_wa_qurani_na_sunna

Mwandishi :

Jafar Subhani

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Eneo la uchapishaji :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

adhana_kwa_mtazamo_wa_qurani_na_sunna

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho “Adhana” cha Sheikh Jafar Subhani. Kitabu hiki kinazungumzia juu ya hitilafu zilizotokea juu ya maneno yanayosomwa katika Adhana. Baadhi ya wanachuoni wanasema kwamba kuna maneno yaliyoongezwa, na wengine wanasema kuna baadhi ya maneno yaliyoondolewa. Ili kujua ukweli wa asili ya Adhana na maneno yake, mwanachuoni Sheikh Jafar Subhani amefanya utafiti juu ya sula hili na kuonesha kwa uwazi na pasina shaka yoyote juu ya asili ya Adhana na maneno yake. Mwanachuoni huyu mtafiti ametumia vyanzo halisi na sahihi katika kulifikia lengo lake hili. Vyanzo hivyo si vingine bali ni Qur’an na Sunna, pamoja na matukio ya kweli ya kihistoria, akili, mantiki na elimu. Kutokana na umuhimu wa maudhui hii tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa mwanga kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili juu ya suala hili ambalo linawatatiza na kujua ukweli wake. Tunamshukuru ndugu yetu Ustadh Hemedi Lubumba kwa kukubali jukumu hili la kutarjumu kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote ambao wameshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki