Drawer trigger

AMALI-ZA-MADINA

AMALI-ZA-MADINA

AMALI-ZA-MADINA

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2013

Eneo la uchapishaji :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

AMALI-ZA-MADINA

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Adabu ‘l-Haramain kilichoandikwa na Sayyid Jawad al-Husaini Aali Ali ash-Shahrudi. Sisi tumekiita, Amali za Madina. Kitabu hiki kinaelezea mambo ya kuzingatiwa kuanzia wakati mtu anapoanza safari kwa ajili ya kufanya ziara (ziyara) katika mji mtukufu wa Madina (yaani Adabu zaZiara). Kila safari ina taratibu zake na madhumuni yake. Kwa hiyo, msafiri hutakiwa kuzingatia utaratibu wa safari hiyo ili kufanikisha madhumuni yake. Safari ya Ziara ina utaratibu na kanuni zake zilizowekwa kisheria, hivyo, mtu anapokwenda mji wowote mtukufu kwa ajili ya Ziara lazima ayazingatie hayo ili afanikishe madhumuni ya safari yake hiyo muhimu. Katika kitabu hiki mwandishi ameelezea kwa lugha fasaha hatua kwa hatua kuanzia mtu kuondoka kwenda kufanya ziara katika mji mtukufu wa Madina mpaka anapomaliza ziara yake na kurudi nyumbani. Mwandishi ameshughulikia kwa kina adabu na amali za kufanya kwa mwenye kufanya ziara Madina tukufu. Hata hivyo, ni matarajio yetu kwamba ataendelea kutufahamisha kuhusu adabu na amali za kufanya katika miji mingine mitukufu insha’Allah.