Drawer trigger

dalili_za_qiyama_na_ubashiri_wa_kudhihiri_imam_mahdi_(a.s)

dalili_za_qiyama_na_ubashiri_wa_kudhihiri_imam_mahdi_(a.s)

dalili_za_qiyama_na_ubashiri_wa_kudhihiri_imam_mahdi_(a.s)

Mchapishaji :

web site ya islam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

dalili_za_qiyama_na_ubashiri_wa_kudhihiri_imam_mahdi_(a.s)

Safina ya msafara wa mwisho wa mwanadamu inakaribia mwisho wake katika dimbwi la hatari ya imani potofu ya kuamini dunia hii tu bila ya kujali Aakhera. Uroho huu umeongezeka katika udanganyifu wetu wa kisayansi kiasi kwamba mwanadamu anataka kuiendesha sayari ya Venus, Mwezi na Jua. Uroho huu umemfanya kiasi cha kuweza kusahau matatizo ya dunia yetu hii. Mashabiki wa utamaduni wameudhalilisha ubinadamu kufikia tabaka la chini kabisa la aibu kiasi kwamba hata kilio cha Baba Adam a.s. pia kitakuwa kimelowana kwa jasho la udhalilisho. Kidhahiri, dunia hii imejaa mwangaza lakini kiza cha ujahiliya kinaenea mbali na kwa mapana. Kizazi cha Shetani kimekwisha tayarisha mipango kamambe ya kulipiza kisasi chake cha kudharauliwa na kizazi cha Mtume Adam a.s. Hali mbaya na machafuko ya matendo ya aina yote ya madhambi ndivyo vilivyosababisha kufungwa milango ya mwanadamu ya kuwa huru. Kivuli cha kiza kikubwa cha misiba ndiyo mambo yanayotia uchungu wa moyo juu ya ubinadamu. “Lakini, mwale wa nuru moja tu wa matumaini katika janga hili la kutokuwa na matumaini ni ile nuru ya nafsi yako (Imam MahdiError: Reference source not found a.s. ) ambayo ipo inang'ara mbali na pazia isiyoonekana. Tunakuomba Ewe Imam Mahdi a.s. ! Udhihiri haraka iwezekanavyo na kwamba ufupishe hayo masaa ya subira yetu kwa ajili yako ingawaje kamwe hatuwezi kupoteza subira zetu kwa ajili yako. ” “Tuombee, udhihirishe yale yaliyo batini na uifanye nuru yako ing'arishe ulimwengu mzima. Dhihirisha maneno ya Allah swt kuwa "Allah swt ataikamilisha nuru yake hata kama makafiri watachukia". Udhahiri wako ndio dalili ya kuja kwa Siku ya Qayama lakini kutokuwapo kwako pia ni yenye maumivu kama Siku ya Mwisho. Wanaadamu tunaoathirika tunakuhitaji mno na mimi ninayo imani kamili ya kuja kwako na mwelekeo mwema katika kudhihiri na njia moja ya kukukaribisha, kwa kunyenyekea ninakitoa kitabu hiki "Qayamat-i-Sughra" mbele yako na natumaini kuwa utanikubalia mimi kama mtumwa wako na hakika hii itakuwa ndiyo uokovu wangu”.