Drawer trigger

ELIMU YA GHAIBU YA MAIMAMU

ELIMU YA GHAIBU YA MAIMAMU

ELIMU YA GHAIBU YA MAIMAMU

Mtarjum :

HARUN PINGILI

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2010

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

ELIMU YA GHAIBU YA MAIMAMU

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ‘Ilmu Aimmah Bi ‘l-Ghayb, kilichoandikwa na Sayyid Abdul Rahim al-Musawi. Sisi tumekiita, Elimu ya Ghaibu ya Maimamu. Ghaibu (ghayb) maana yake - yasioonekana. Sharti moja la imani katika Uislamu ni kuamini yasiyoonekana ambayo kwa kweli ni mengi sana, lakini kwa kutaja machache ni kama vile, malaika, majini, Pepo, moto wa Jahannam, roho, n.k. Hivi vyote havionekani katika macho yetu lakini vipo na lazima tuamini hivyo. Qur’ani Tukufu inasema: “Hicho ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wamchao (Mungu), ambao huyaamini yasiyoonekana...” (2: 2-3). Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kwa kina maana halisi ya ghaibu kwa kutumia vyanzo vitukufu - Qur’ani Tukufu, Sunna na hoja za kielimu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Harun Pingili kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa sana kwa wasomaji wetu na Waislamu wote kwa ujumla.