Drawer trigger

Hayyaalla-khayril-Amali-katika-Adhana

Hayyaalla-khayril-Amali-katika-Adhana

Hayyaalla-khayril-Amali-katika-Adhana

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2011

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Hayyaalla-khayril-Amali-katika-Adhana

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "Hayya’alla khayril A’Mali" Kitabu hiki kimeshughulikia tamko hili la Adhana ambalo limo katika Adhana ya Mashia na ambalo halimo katika Adhana ya Masunni. Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.