Drawer trigger

HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI

HISTORIA YA CHANZO  CHA MAWAHHABI

HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI

Mwaka wa uchapishaji :

2003

Idadi ya juzuu :

1000

Chapisha nambari :

Toleo ya Sita

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI

Kuanzia mazungumzo yangu, natanguliza aya ifuatayo kama dibaji ya maudhui yenyewe. Mwenyezi Mungu Mwenye Rehma amesema katika Qur’ani tukufu kuwa: “Akasema: Hakika wafalme wanapouingia mji, wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili; hivyo ndivyo wanavyofanya”. (27:34) Aya hii inatoa ujumbe kwa Waislamu ulio muhimu sana. Inaeleza kwamba unapotokea ufalme usiotosheka na milki yake na ukawa na nia ya kutaka kupanua himaya yake na mipaka yake, basi daima ufalme kama huu hauwezi kuzingatia kanuni za haki katika nidhamu yake. Na hapo ufalme huo hupotoka na kuanza kuvamia nchi nyingine na kuiteka miji yake na kufanya ufisadi ikiwa ni pamoja na kuharibu mali na kuhilikisha maisha ya wanadamu. Kwa kuwa Mawahhabi historia yao inaonyesha kutokana kwao na mambo ya ufalme na mauaji hapana shaka kuwa aya hii inazungumzika katika fitna yao.