Drawer trigger

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislamu

Huduma ya Afya katika Uislamu

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2011

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Huduma ya Afya katika Uislamu

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ar-Ri’ayatu ‘s-Swihiyyah Fi ‘l-Islam kilichoandikwa na Jopo la Wataalamu la Taasisi a Balagha. Sisi tumekiita, Huduma ya Afya katika Uislamu. Afya ya mwili kwa mwanadamu ni kitu muhimu sana. Ili mwanadamu aweze kuyajenga maisha yake na kuwa bora kimwili, lazima awe na afya bora, na sio tu kwa ajili ya kuendesha maisha yake, bali pia bila afya nzuri mtu hawezi kutekeleza ibada zake sawasawa jinsi inavyotakiwa kuifanya. Hivyo, kama Uislamu ulivyo kwamba ni dini na ni mfumo kamili wa maisha, umeelezea kwa kina huduma ya afya, yaani mtu akiwa nini ili ajipatie afya njema. Waandishi wa kitabu hiki wameelezea mambo mbalimbali ambayo yanapaswa kufanywa kwa ajili ya afya ya mtu binafsi na ya jamii kwa ujumla. Katika maelezo yao wamezingatia Qur’ani Tukufu, Sunna pamoja na mafundisho ya Maimamu Watukufu. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.