Drawer trigger

Imam Hassan Mfumo wa Kejenga Jamii

Imam Hassan Mfumo wa Kejenga Jamii

Imam Hassan Mfumo wa Kejenga Jamii

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2014

Eneo la uchapishaji :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Imam Hassan Mfumo wa Kejenga Jamii

Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Imamu ‘l-Hasan wa ‘l-Bana’a ‘l-Ijtima’iy kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita, Imam Hasan na Mfumo wa Kujenga Jamii. Imam Hasan (a.s.) ni mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kutokana na binti yake mpenzi, Fatima Zahra (a.s.) na baba yake Imam Ali bin Abu Talib (a.s.). Imam Hasan (a.s.) ni Imamu wa pili katika Maimamu wa Ahul Bayt (a.s.). Ni ukweli ulio dhahiri kwamba Maimamu hawa wanaotokana na Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wateule wa Mungu, na maisha yao ni mfano wa kuigwa katika jamii ya wakati ule na wakati huu na wakati ujao. Katika kitabu hiki tutaona jinsi Imam Hasan (a.s.) alivyoishi na jamii iliyomzunguka kwa upole, unyenyekevu na huruma, na jinsi alivyokuwa akiwahudumia wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali bila ubaguzi wowote au kujali kama ni maadui au wafuasi wake. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutoka na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapishakitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake