Drawer trigger

IMAM MAHDI (A) NI TUMAINI LA MATAIFA

IMAM MAHDI (A) NI TUMAINI LA MATAIFA

IMAM MAHDI (A) NI TUMAINI LA MATAIFA

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2015

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

IMAM MAHDI (A) NI TUMAINI LA MATAIFA

Kitabu ulichonacho mikononi mwako kimetarjumiwa kutoka kitabu cha Kiarabu kwa jina la, al-Imamu ‘l-Mahdi ‘Alaysi ‘s-salaam Amalu ‘sh-Shu’uub, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita, Imam Mahdi (a.s.) ni Tumaini la Mataifa.
Mojawapo kati ya kanuni za imani (itikadi) ambazo Qur’ani Tukufu hudai na kuthibitisha ni kanuni ya imani katika Imam Mahdi (a.s.) na sifa zake. Qur’ani Tukufu inasema: “...Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote...” (6:38). Katika aya nyingine, Kitabu cha Allah kinasema: “...na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu...” (16:89).
Ili kuelezea msimamo wa Qur’ani kuhusiana na imani ya Umahdia (mahdawiyyah), hadithi nyingi zimesherehesha aya hizi kupitia minyororo ya wasimulizi wa Shia na halikadhalika wa Sunni. Hadithi hizi husema kwa uwazi kwamba aya hizi huelezea kuhusu Imam Mahdi (a.s.). Kitabu ambacho kimekusanya kwa ubora aya za Qur’ani ambazo huzungumzia kuhusu Imam Mahdi (a.s.) katika mwanga wa hadithi na riwaya za Kisunni kinaitwa, al-Mahdi Fi ‘l-Qur’an kilichoandikwa na mwanachuoni mwenye kuheshimiwa, Sayyid Sadiq Shirazi katika mwaka wa 1978.
Qur’ani ina vipengele mbalimbali vya kudhihiri tena, Ughaibu na pia sifa za Mtukufu Mahdi (a.s). Vyote hivi vikiwa vinakubaliwa na wote, wanavyuoni wa Kishia na halikadhalika wanavyuoni wa Kisunni ambao ni wenye mamlaka zaidi na wa kuaminika. Aya za Qur’ani kuhusu kujitokeza tena na mapinduzi ya Imam Mahdi (a.s.) - imani ya kawaida kwa Ahli Sunna pia - hutaja sifa nne na malengo ya utawala wa ulimwengu wa Imam Mahdi (a.s.):  

Kusimamisha utawala ya ulimwengu mzima.
Madaraka kamili kwa dini ya Uislamu.
Mazingira ya usalama kamili na amani.
Uangamizaji wa ushirikina (shirk).


Imam Mahdi ambaye katika utamaduni wa Kiswahili hujulikana pia kwa jina la “Muhudi” atajidhihirisha tena kutoka Ughaibu na kusimama wakati wa kipindi cha mwisho na utaujaza ulimwengu kwa uadilifu na usawa kama ambavyo utakuwa umejaa dhulma na ukandamizaji. (Kifayatu ‘l-Athar, uk. 12). Atasafisha uso wa ardhi kutokana na aina zote za dhulma na udikteta na kuitakasa kutokana na aina zote za maovu.
Hii ni moja kati ya kazi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Al- Itrah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeona ikichapishe kitabu hiki chenye hazina kubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili.
Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufaika vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.
Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Hasan Musa as-Saffar kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah amlipe kila kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunamshukuru Ustadh Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Mwenye kujazi amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera pia, bila kuwasahau
na wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera pia.