Drawer trigger

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur'ani Tukufu

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur'ani Tukufu

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur'ani Tukufu

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2008

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur'ani Tukufu

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la, Mafhumu ‘l-La’na wa ‘s-Sabb fi ‘l-Qur’ani l-Karim. Sisi tumekiita, Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu, kilichoandikwa na Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani. Kitabu hiki, Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu, ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni huyu wa Kiislamu. Kitabu hiki ni majibu kwa wale wanaowashutumu Mashia kwamba wanawatukana masahaba, shutuma ambazo zimekuwa zikitolewa kwa karne nyingi sana licha ya wenyewe Mashia kukana shutuma hizi kwa nguvu sana. Kwa bahati mbaya, shutuma hizi zilikuwa zikijibiwa kwa lugha za kigeni, hususan Kiarabu na Kiingereza, na kuwaacha wasomaji wa Kiswahili wasijue chochote kuhusu suala hili. Basi kitabu hiki ni moja ya vitabu vinavyotoa majibu ya shutuma hizo kwa lugha ya Kiarabu, ambacho tumekitarjumi kwa lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.