Drawer trigger

HISTORIA YA UISLAMU (JARIDA LA KWANZA)

HISTORIA YA UISLAMU  (JARIDA LA KWANZA)

HISTORIA YA UISLAMU (JARIDA LA KWANZA)

Mwaka wa uchapishaji :

2003

Chapisha nambari :

Toleo ya Tatu

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

HISTORIA YA UISLAMU (JARIDA LA KWANZA)

Marehemu Nawwab Sheikh Ahmad Husain Khan Bahadur, O.B.E., wa Paryawan (Bara Hindi) katika mwaka 1920 A.D. alitunga historia ya Uislamu na akaipa jina ‘Taarikh-e-Ahmadi.’ Historia hiyo ilikuwa namna ya pekee, kwa sababu mwandishi huyo hakutumia hata neno moja kutokana kwake; bali alinakili sehemu zenye kufaa kutokana na vitabu mbali mbali zijulikanazo na thabiti za historia, hadithi, na habari za maisha ya watu. Maneno aliyoongeza yeye katika kitabu hiki ni kihusishi (preposition) tu, maneno yenye kuunganisha kama, ‘na’, ‘kwa’, ‘baadaye’, ‘tena’, na kadhalika, ili kuunganisha fungu la maneno. Kitabu hiki kimepigwa chapa mara nyingi katika Bara Hindi na Pakistani. Katika mwaka 1965 A.D. tafsiri (kwa ufupi) ya sehemu ya mwanzo kitabu hiki kwa lugha ya kiingereza kimepigwa chapa Mumbai na ikapewa jina “Gems of Islam History”. Kitabu hiki chetu ni tafsiri ya “Gems of Islamic History”, lakini hichi kimesahihishwa kutokana na kile kitabu cha asili. Kitabu hiki chaeleza matukio ya maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); lazima tujulishe hapa kwamba maelezo haya ya maisha si ya kinaganaga. Msomaji ataona hakika ni kitabu chenye faida sana kwa sababu mhariri na mfasiri hawakukusudia kuthibitisha au kukanusha kitu chochote kwa kupotoa jambo la kweli la historia, kama wanavyofanya watungaji wengi siku hizi. Kitabu chetu hiki kinaonesha hasa maneno ya vitabu vya asili na kumwacha msomaji awe huru kufikiria mawazo yake binafsi. Na kwa kuwa kitabu hiki cha pekee kisicho na kifani, Bilal Muslim Mission imechikuwa fursa ya kuwatumikia wa Afrika ya mashariki ili wajipatie maandishi halisi yawanachuoni waliotangulia wa zamani. Natumai kitabu hiki kitapendezewa kama vilivyopendwa vitabu vyetu vingine vya mbele.