Drawer trigger

UHARAMISHO WA KAMARI

UHARAMISHO  WA KAMARI

UHARAMISHO WA KAMARI

Mwaka wa uchapishaji :

1996

Idadi ya juzuu :

2000

Chapisha nambari :

Toleo la kwanza

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam - Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

UHARAMISHO WA KAMARI

Ninamshukuru Allah swt pamoja na Mtume Mtukufu s.a.w.w. na Ahli-Bayt Toharifu a.s. kwa kunijaalia neema hii ya kuweza kukitarjumu kijitabu hiki juu ya maudhui haya ya kamari ili kuweza kuwafaidisha wanaadamu wenzetu ili nao waweze kujiokoa na janga hili kubwa linaloangamiza watu pamoja na famili zao zikiteseka kizazi baada ya kizazi. Mimi binafsi nimewaona wajukuu ambao mpaka leo wanateseka kwa ajili ya madhambi ya mababu zao. Vile vile hapa mjini kwetu nilikuta watu wenye mapesa wakiongoza katika makundi yao ya kucheza kamari kwa mapesa, yaani Waislamu ndio waliokuwa wakiendesha madanguro hayo. Kwa hakika nilijaribu kutoa makala juu ya uharamisho wa kamari, lakini niliyokumbana nayo yananitosha, na wala sina haja kuyaelezea hapa. Ndipo hapo nilipoona umuhimu wa kukitayarisha kijitabu hiki juu ya uovu wa kamari. Makusudi yangu ni kutaka kuwasaidia na kuwaelimisha watu juu ya uovu huo wa kamari. Ni mategemeo yangu kuwa maudhui haya yatatufaidisha na kutuongoza katika njia njema yenye kujenga maisha yetu na ya jamii nzima kwa ujumla.