BIBLIA NENO LA MUNGU

BIBLIA NENO LA MUNGU

BIBLIA NENO LA MUNGU

Publication year :

1987

Publish number :

Chapa ya tatu

Number of volumes :

1

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

BIBLIA NENO LA MUNGU

Hii  ni  tafsiri  ya  Kijitabu  Kilichoandikwa  kwa  lugha  ya  Kiarabu,  Kilichoandikwa  na Ayaatullah Seeyyid Muhammed Mahdi Shirazi wa Karbala. Tafsiri yenyewe ilifanywa na Seyyid Muhammed Mahdi Shushtari wa Unguja. Sura nyingi Zilichapishwa kwa mfulizo katika gazeti letu. Sauti ya Bilal na zilipendeza sana. Sasa kijitabu hiki kimechapishwa ili Kuwarithisha zaidi wasomaji wetu. Hatuna  budi  kutamka  hapa  kuwa  mujibu  wa  imani  yetu,  Mitume  wote  waalikuwa wametumwa na Mwenyezi Mungu Kuwaongiza watu katika njia iliyo sawa. Waalifanya hivyo kwa kuhubiri wema wao mkuu na kwa matendo yao maadilifu. Kufanya  hivyo  iliwapasa  wawe  waongofu  zaidi,  waadilifu  na  kuwa  wakamilifu  katika uchaji  wao  kwa  Mwenyezi  Mungu.   Wasingeweza  kusema  uwongo  iwapo  wao walifundisha  watu  kusema  kweli.Wasingeweza   kumwomba  Miungu,  iwapo  wao waliwataka watu kumwomba Mungu Aliye Mmoja tu, na kadhalika. Hata  hivyo,  Biblia  inasingizia  zote  za  maovu  na  madhambi  kwa  Mitume  hao.   Ama viongozi wa Kiyahudi na Wakristo walikuwa na madhambi makubwa kabisa, la sivyo, basi ni makosa ya Biblia yenyewe (inayoaminiwa kuwa si maandishi ya Musa wala Isa a.s) Kwa hiyo, ni juu ya msomaji mwenyewe kuteua yapi yanayomfaa na yapi yasiyomfaa. Syed saeed Akhtar Rizvi