TUNDA LA KHERI
TUNDA LA KHERI
(0 Kura)
(0 Kura)
TUNDA LA KHERI
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Huruma. Salawat juu ya Mtume, Hazrat Muhammad (SAW) na kizazi chake na juu ya wafuasi wake waaminifu. Qur’an pamoja na Hadith zinasisitiza Ilm na Taqwa kuwa sifa asili za Muislamu. Mtu mwenye elimu lakini akawa si mwenye vitendo, ni kama mfano wa shamba lililojaa magugu; na mcha Mungu mwenye kufanya ibada lakini akawa hana elimu, ni kama kipofu atafuate kwa kupapasapapasa katika giza. Historia ya Uislamu na ya Waislamu imejaa matendo na matukio ambayo yanatoa mifano ya mchanganyiko wa furaha kama huu. Tumefanya uchaguzi wa mifano kama haya kutoka katika asili zijulikanazo vizuri. Hizi ndizo asili tulizochukulia mifano iliyomo kitabuni:
“Tuhaful Uqool” kilichoandikwa na Abu Muhammad Al-Harrani;
“Biharul Anwar” kilichoandikwa na Allamah Majisi; “Al-Amthalun Nabawiyyah” kilichoandikwa na Muhammad Al-Gharawi na juu ya vyote, “Dastan—e—Rastan” kiljchoandikwa na mwanachuoni mkubwa wa wakati huu wetu, As-Shaheed Murtaza Mutahhari.
Kwa wanaofundisha Akhlaqiyyat katika madrassa zetu na pia kwa wenye kuhutubia na Zakireen ni matumaini yetu kuwa kitabu hiki kitakua msaada mkubwa kwao.