RISALATUL HUQUQ
RISALATUL HUQUQ
Interpreter :
Publisher :
(0 Kura)
(0 Kura)
RISALATUL HUQUQ
Wajibu na haki ya awali na ya asili ni haki ya Mwenyenzi Mungu kwako, kwani yeye ndiye aliyekuumba na kuweweka hapo ulipo,haki ya Mwenyezi Mungu ndio haki kuu na haki nyingine ni matawi ya haki hiyo, haki nyingine ni haki yako wewe ambayo inakuhusu wewe na mazingira yako yote kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu mtukufu, amevipa viungo vyako haki na misingi maalum ya kuifuata; macho yana haki yake,masikio yana haki yake,ulimi una haki yake,mikono ina haki yake,miguu ina haki yake,tumbo lina haki yake na tupu zina haki yake, viungo hivi saba ndiyo viungo ambavyo kwa kawaida mwanadamu huvitumia katika matendo na amali zake za kila siku.
Kisha Mwenyezi Mungu amezipitia amali zako haki kwako, sala ina haki yake kwako, saumu ina haki yake kwako, sadaka ina haki yake kwako, hadiya ina haki yake kwako na matendo yako mengine yote, Mwenyezi Mungu mtukufu, ameyawekea haki zake kwako.
Kisha tunahama kutoka kwenye haki zako kuelekea kwenye haki za wenzako, ambapo katika hao kuna wenye haki za wajibu kwako, mfano wa haki za Mitume na Maimamu kwako na haki za ndugu jamaa na rafiki zako.
Haki hizi tulizo zitaja ndio asasi na msingi waa haki za binadamu, na haki nyingine zote zinatokana au ni sehemu ya haki hizi:
Haki za viongozi; ziko katika mafungu matatu: haki za viongozi wako, haki ya walimu wako na haki za walezi wako.
Haki za raia; ziko katika mafungu matatu: haki ya raia kwa kiongozi, haki ya mwanafunzi kwa mwalimu, na haki ya watu kwa walezi wao.
Watu walio chini ya mamlaka yako kama vile watumishi, mke na watoto wote wanahaki zao kwako,
Ndugu zako na watu wako wa karibu pia wanahaki zao kwako, ambapo mwenye haki zaidi kwako ni mama yako, kisha baba yako, kisha kaka na dada zako na kisha haki za ndugu wengine, ambapo aliyekaribu zaidi ana haki zaidi.
Kisha kuna haki ya wakuu wako wa kazi, haki ya wafanya kazi wako, haki ya waliokufanyia hisani, haki ya muadhini, haki ya imamu na haki ya maamuma wenzako.
Kisha kuna haki ya jirani, haki ya swahiba, haki ya mshirika, haki ya tajiri, haki ya mtu unayemdai, haki ya anayekudai, haki ya unaoishi nao, haki ya mshauri na haki ya mwenye kukuomba ushauri.
Kisha haki ya mwenye kukuomba nasaha na haki ya mtoa nasaha na kunasihi, haki ya wakubwa zako na haki ya wadogo zako, haki ya mwenye kukuomba na haki ya unayemuomba, haki ya aliyekutendea wema na aliyekutendea ubaya, ima kwa makusudi au bahati mbaya, haki ya waislamu wenzako na haki ya wasio kuwa waislamu kwako, haki kwa majanga na mabalaa yanayowasibu watu.
Basi ni faida iliyoje kwa yule mwenye kutekeleza haki za binadamu na kutekeleza wajibu wake aliyowekewa na Mwenyezu Mungu mtukufu.
Kitabu hiki kinaelezea haki za binadamu kutoka katika mafunzo ya imam Sajjad ambaye ni maarufu kama Imam Zainul Abidin ambaye ni mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w[1] ambaye pia ni imamu wa nne wa dhehebu la kiislamu la Shia ithna asharia.
Katika kitabu hiki Imam Zainul Abidin ametufundisha haki za binadamu hamsini.
Natumai kitabu hiki kitakuwa ni muongozo sahihi kwa wapenda haki kote ulimwenguni.
[1] S.a.w = Swalla llahu alai wa alihi.