UJUMBE WA IMAM KHOMEINI KWENYE MAADHIMISHO YA MILENIA YA NAHJU ’l-BAlÃGHAH

UJUMBE WA IMAM KHOMEINI KWENYE MAADHIMISHO YA MILENIA YA NAHJU ’l-BAlÃGHAH

UJUMBE WA IMAM KHOMEINI KWENYE MAADHIMISHO YA MILENIA YA NAHJU ’l-BAlÃGHAH

Publish location :

Dar-es-Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

UJUMBE WA IMAM KHOMEINI KWENYE MAADHIMISHO YA MILENIA YA NAHJU ’l-BAlÃGHAH

Kijitabu hiki kimebeba ujumbe wa Ayatullah al-Uzma Imãm Khomeini (Mwenyezi Mungu ampe daraja la juu Peponi), muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; Ujumbe alioupeleka kwenye Mkutano wa kusherehekea kupita miaka elfu moja ya mtungo ya Nahju ’l-Balaghah, uliofanyika mjini Tehran mwezi Mei, 1981. Ujumbe huu, licha ya ufupi wake unavuta hisia katika nyanja nyingi za kitabu; hisia ambazo zinalenga katika masuala ya Kidini, Irfani, Falsafa, Maadili, Elimu, Jamii, Ulinzi, Utamaduni na zinginezo. Mkusanyaji wa Nahju ’l-Balaghah, as-Sayyid ash-Sharif ar-Radhi (359 - 406 A.H.) ameuweka Ulimwengu wa Kiislamu chinni ya ufadhili wake kwa kuweka katika mikono yao Kioo ambacho wataona taswira halisi ya Mzungumzaji na Mwandishi wa Hotba, barua na Hadithi hizi ambaye ni Kiongozi wa Waumini ‘Ali ibn Abi Talib (a.s.). Hivi sasa Mheshimiwa Kiongozi wa Kitengo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kushirikiana na Bilal Muslim Mission of Tanzania na Ahlul~Bayt (a.s.) Assembly of Tanzania wanachapisha tafsiri ya Kiswahili ya Ujumbe huo kwa ajili ya Semina ya Nahju ’l-Balaghah itakayofanyika Dar-es-Salaam tarehe 28 na 29 Septemba, 2001, kwa lengo la jamii izungumzayo Kiswahili kupata nafasi ya kuzingatia kutafakari kuhusu ujumbe huu muhimu wa Imãm Khomeini (R.A.) na kupata mwongozo kutokana nao.