Drawer trigger

Mtindo wa Maisha

Mtindo wa Maisha

Mtindo wa Maisha

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Mtindo wa Maisha

Sisi tunaamini kwamba, maktaba (mafunzo) yenye uhai ya Uislamu na maarifa ya Kiislamu yanajumuisha na kukidhi mahitaji yote ya mwanadamu mpaka siku ya Kiyama na yametoa na kuweka bayana utamaduni na mtindo wa maisha.

Hii leo vyombo mbalimbali vya habari vya Magharibi na satalaiti za maadui vimeanzisha vita laini (soft war) na hujuma kubwa katika engo mbalimbali za mtindo wa maisha wa Kiislamu. Moja ya njia za kukabiliana na hujuma hii kubwa ya maadui wa Uislamu, ni kutambulisha mtindo wa maisha ya Mtume (SAW) na Ahlul Bait wake (AS).

Mtindo wa maisha wa waja hawa watukufu ni ruwaza njema na kiigizo cha hali ya juu kwa ajili ya maisha ya mwanadamu katika kipindi chote cha historia ya mwanaadamu ambao hautakaririwa tena.

Kwa msingi huo, kuegemea shakhsia ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (AS) na kufuata kwa njia sahihi mtindo wa maisha yake, kuna ulazima wa kutanguliza mbele sira na matamshi yake ili iwezekane kufikia lengo la mtindo wa maisha wa mtukufu huyo. Yaani kuna haja ya kuifahamu na kuielewa sira na mwenedo wa maisha yake.

Kitabu hiki kinatoa majibu ya maswali ya wasomaji wapendwa kuhusiana na mtindo sahihi na mzuri wa kuishi kwa kustafidi na turathi ya miongozo ya Imam mwema, mtukufu Imam Ridha (AS) na kinabainisha namna ya kuishi kiumini katika kivuli cha mawasiliano na Mwenyezi Mungu na kiumbe wake.

Tuna matumaini kwamba, kwa kuyafanya maisha ya Kiradhawi (ya Imam Ridha) kuwa kigezo chetu, tutaweza kuwa na maisha mazuri na hivyo kufuta na kuondoa kabisa katika maisha yetu kigezo cha namna ya kuishi cha kiajinabia (kigeni).