BANGI YAUA NA YAIMARISHA UKOLONI

BANGI YAUA NA YAIMARISHA UKOLONI

BANGI YAUA NA YAIMARISHA UKOLONI

Interpreter :

Hassan Ali Mwalupa

Publish location :

Tehran Islamic Republic of Iran

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

BANGI YAUA NA YAIMARISHA UKOLONI

"Moja... Mbili... Tatu... "Aa! Nzuri kabisa! Tumekuwa malaika, hamhisi hivyo?" "Ndiooo!! Ndiooo!!" "Basi njooni turuke mbinguni." "Hiyo ni fikra nzuri. Haya na turuke! "Moja... Mbili. .. Tatu..." Vijana watano wanachupa kutoka ghorofa ya kumi na tisa, wanakatika vipandevipande na nyama na mifupa kutawanyika. Mama watano wanaingiwa na majonzi ya vijana wao ambao baada ya kuvuta bangi walipandwa na nishai na walijiona kuwa ni malaika na kwamba wangeweza kuruka. Wasichana na wavulana huvua nguo zao hadharani na kufanya vitendo vichafu, kisha hucheza wakiwa uchi huku watoto wakiwazunguka na wakiwatupia maganda ya ndizi na kuwacheka! Kijana asiyezidi umri wa miaka kumi na tano hukaa kwenye baraza la nyumba yao iliyoelekea mashariki, akilikodolea macho jua kwa muda wa masaa mengi huku akiimba: "Mwezi weee!! Mwezi weee!!. . ." mpaka huchoka kiasi ambacho huwa yu hoi kabisa. Hupelekwa hospitali na kuonekana kuwa amepofuka macho kiasi ambacho hawezi kutibiwa. Katika siku moja asubuhi, mtu mmoja mwenye umri wa miaka hamsini alitangaza kwamba alikuwa nabii wa mwisho, na kwamba utume wake unahusu wajibu wa "ibada ya mwanamke!" Usiku wa manane wa siku hiyohiyo, watu wakasikia sauti ya ugomvi ikifuatiwa na sauti ya kuugua. Asubuhi ilipopambazuka, ikabainika kwamba mtu huyo amemwua mke wake usiku ule. Hivyo ndivyo bangi, kasumba na vileo vingine vinavyowafanya watu! Na hiyo ndiyo hali waliyoizoea watu katika nchi ambazo vileo hutumiwa kwa wingi sana, kama vile Marekani, Sweden na Thailand. Afyuni, heroini au bangi, kwa mfano, humpumbaza mtu na ikampa nishai akawa anawaza mawazo mbalimbali mpaka kujifikiria kuwa yeye ni malaika, nabii au kwamba ana ahadi kuutongoza mwezi kumbe ni jua! Kisha heroini humfanya mtu afanye vile mawazo yake yanavyompumbaza na kumwamrisha; hujaribu kuruka kutoka kwenye paa ya nyumba kuelekea mbinguni, na matokeo yake huanguka chini na kuvunjikavunjika mifupa yake na kufa. Au humfanya aliimbie jua nyimbo za mapenzi huku akilitazama kwa muda mrefu mpaka akapofuka macho. Au anawalingania watu wamwabudu mwanamke wakati wa asubuhi, kisha humwua mkewe usiku wa manane. Namna hii ndivyo heroini inavyoondoa utu wa mtu. Lakini je, ni heroini tu ndiyo inayoondoa utu? Je, pombe nayo inamwathiri vipi mlevi? Tukiachilia mbali madhara yanayoletwa na pombe kwa maini na mishipa ya fahamu (neva) na jinsi athari yake ilivyo mbaya, utaona kwamba daktari humwuliza mgonjwa wa ini, macho au neva:  "Je, unakunywa pombe?" Akikataa humwuliza: "Je, baba yako vipi?" Akikataa humwuliza: "Je, babu yako alikuwa akilewa?" Akisema ndiyo, husema: "Huo ni ugonjwa wa kurithi!" Tuyawache yote hayo na tuzungumzie matokeo yanayoletwa na ulewaji katika jamii. Hapana shaka kwamba pombe ina ladha nzuri kwa mnywaji. Na tukichukulia kwamba pombe haidhuru siha ya mtu na akili yake na kwamba athari yake ni ya muda tu, basi hapo tujiulize, je, athari ya jamii ikoje? Je, jamii inalazimika kuvumilia athari za hatari kwa sababu mtu fulani anapata "utamu wa ulevi?" Kazi ya wizi pia ina Iadha kwa mwizi, lakini athari yake ya kijamii ambayo huharibu mizani ya uadilifu ndiyo inayotufanya tumwadhibu mwizi.