NDOA KATIKA ISLAM
NDOA KATIKA ISLAM
Author :
(0 Kura)
(0 Kura)
NDOA KATIKA ISLAM
Ndoa Katika Islam Kimekusanywa na kutarjumiwa na Amiraly M. H. Datoo Bukoba - Tanzania Namshukuru Allah swt, Mtume Mtukufu s.a.w.w. pamoja na Ahli Bayt Tukufu a.s. kwa kunijaalia niweze kufanikisha juhudi zangu hizi katika kukitayarisha kitabu hiki juu ya maudhui haya ya “Ndoa katika Islam”. Mnamo mwezi April 1994 nilifanyiwa operesheni ya appendix huko Dar es Salaam, na wakati bado nikiwa ninauguliwa, nilikianza kitabu hiki. Na baada ya kukusanya yakutosha nilikiacha, na kuendelea na maudhui nyinginezo katika kufanyia utafiti. Na takriban tarehe 28 mwezi Julai 1995 nilibahatika kumtembelea Chief Missionary wa ‘Bilal Muslim Mission of Tanzania’, Hujjatul-Islam Sayyid Saeed Akhtar Rizvi na katika mazungumzo yetu kulitokezea mazungumzo juu ya kitabu cha “Ndoa katika Islam”.. Na nilimwambia kuwa nilikuwa nimekifanyia kazi kiasi fulani. Kwa hakika yeye alivutiwa mno, na kuniomba nikikamilishe haraka iwezekanavyo kwani alikuwa akihitaji kuchapa kitabu juu ya maudhui hayo. Nami baada ya kurejea kwangu Bukoba, tarehe 2.8.1995 nilikalia kitabu hiki na kuweza kukikamilisha vyema kwa uwezo wangu mdogo hadi leo tarehe 28.8.1995. Hivyo ni matumaini yangu kuwa, utafiti nilioufanya kwa kiasi hicho kidogo, kitasaidia katika ndoa zetu na masuala yanayohusiana nayo na wengi wetu tutaweza kujirekebisha ili kuweza kujipatia matunda bora kabisa katika maisha ya ndoa. Hata hivyo nitapenda kupokea maoni na ushauri na masahihisho kuhusu maudhui ya kitabu hiki kwa ujumla ili niweze kuendeleza sura zinginezo ambazo sikuzigusia, ingawaje ni nyingi.