JE, MUNGU ATAONEKANA? [Mjadala wa Kiitikadi, na Kifalsafa kwa mujibu wa Qur’ani na Sunnah]
JE, MUNGU ATAONEKANA? [Mjadala wa Kiitikadi, na Kifalsafa kwa mujibu wa Qur’ani na Sunnah]
Author :
Publish location :
ZANZIBAR TANZANIA
(0 Kura)
(0 Kura)
JE, MUNGU ATAONEKANA? [Mjadala wa Kiitikadi, na Kifalsafa kwa mujibu wa Qur’ani na Sunnah]
Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa dunia hii, Rehma na amani zimshukie Mtukufu Mtume (s.a.w.) pamoja na ahli zake wote. Qur’ani tukufu inawataka wanaadamu kutafakari na kuzingatia hasa katika vile vilivyoumbwa na Mungu ili waweze kuzielewa siri za maumbile. Mwanadamu anatakiwa aifikirie hali yake, matendo yake na nafsi yake. Kuzingatia matukio ya kihistoria kunapelekea kuweza kuelewa asili ya mambo yalivyo. Hivyo, Uislamu unaiona tauhidi ambayo, ndiyo kielelezo hasa cha upweke wa Mungu, kama jambo la msingi ambalo ni wajibu kulitafakari na kulizingatia. Imepokewa kutoka kwa Abu Abdillah (a.s.), kuwa siku moja Imam Ali (a.s.) alipokuwa anahutubu juu ya Mimbar ya msikiti wa mji wa Al-Kufa, huko Iraq, mtu mmoja aliyeitwa Daalabu alisimama na kumuuliza haya: “Ewe Amiirul-muuminiin, umewahi kumwona Mola wako?” Imam akasema: “Ole wako ewe Daalab, mimi siwezi kumuabudu Mungu nisiyemuona”. Daalab akasema: “Ewe Imam, umemuonaje?” Imam akajibu kwa kumwambia: “Ewe Daalab, elewa kuwa macho hayawezi kumuona kwa kumtazama bali nyoyo ndizo zinazomuona kutokana na ukweli wa imani…” 1 ُ“Macho hayamfikii kumuona bali Yeye anayafikia macho, naye ni Mwenye kujua (ya ndani) Mwenye khabari.”2 Upweke wa Mwenyezi Mungu ni nadharia isiyo shaka na ipo haja ya 1 Kutoka kitabu “A Shiite Anthology” cha Allamah Sayyid Muhammad Husayn Tabatabaiy, uk. wa 38-39. 2 Suratul An’aam, aya ya 103 2 kueleza mipaka ya asili ya kumpwekesha Allah (tawhid) na ile mipaka inayopelekea ushirikina (shirk), jambo hili linahitajia vielelezo na mazingatio makubwa kwa vile ndio hasa mzizi mkuu wa dini yenyewe. Qur’ani imewasisitiza watu kutafakari kwenye maumbile na maajabu yake ili wapate kumuelewa Muumba hasa wa maumbile hayo. Mara nyingine Qur’ani huashiria hayo kwa kusema: ِ“Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na katika kupishana kwa usiku na mchana, na katika vyombo vipitavyo baharini kubeba yale yenye faida kwa watu, na katika maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni ambayo kwayo ameihuisha ardhi baada ya kuchakaa, kisha akaeneza humo aina zote za wanyama, na katika mabadiliko ya pepo na mawingu yaliyoamriwa kupita baina ya mbingu na ardhi; bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wenye kuzingatia.” 3 Mwislamu anatakiwa azingatie haya yote ili aelewe uwezo, sifa, na hatimaye dhati 4 ya Mola wake. Inasikitisha kuona kuwa Waislamu sasa wameiacha falsafa hii ya kutafakari kwa kutumia vipaji na akili zao.5 3 Suratul Baqarah, aya ya 106 4 Dhati ya Allah haieleweki. Kwa hivyo, jua ndugu msomaji kwamba makusudio yangu juu ya kuijua dhati ya Allah, ni vile kutokuijua kwani, kama ilivyosemwa, kutokumdiriki Allah ndio kumdiriki kwenyewe. 5 Sikusudii kusema kwamba tuitangulize akili kuliko Sharia, bali nakusudia kusema kwamba tutumie akili katika kuisoma Sharia, kwani Sharia haigongani na akili. Naam! Yako mambo ambayo akili ya binaadamu haina uwezo wa kuyafahamu. Mambo haya ni baadhi ya mambo ya Sharia: si mambo ya kiakili. Mfano wa hayo ni kama vile ni kwa sababu gani tusali rakaa mbili alfajiri na nne adhuhuri; kwa nini tuzunguke al-Ka’aba n.k. Lakini, tena, elewa kwamba kuna tofauti baina ya mambo ambayo yanagongana na akili na mambo ambayo akili haina uwezo wa kuyafahamu. Mambo hayo tulioyataja hapo si kwamba yanagongana na akili bali ni mambo ambayo akili ya kiumbe haiwezi kuyafahamu. Ama mambo yanayohusiana na sifa za Allah ni mambo yanayofahamika kiakili. Huoni kwamba akili timamu haihitaji andiko ili kujua kuwa Allah ndiye Muumba, Muweza, Mwenye elimu n.k. Matokeo ya jambo hili ni kwamba kumepatikana watu wanaokataa kabisa kutumia akili zao katika Uislamu. Kwa ajili ya hayo kukapatikana Waislamu wanaoitwa “ahlu-dhwahiri”, ambao ni wale waliozichukua hadithi, aya na ibara nyingine kama zilivyo katika maana yake ya juu juu au ya dhahiri. Kuna wengine huitwa “ahlul-hadith”. Wengine wakajiita “as-salafiyyah”. Bali hawa walikataa hata kuzifanyia taawili baadi ya aya za Qur’ani ili kupata maana sahihi inayokubaliana na fikra ama akili zilizoumbwa na Mungu. Hayo ndio mambo yaliyotukumba. Qur’ani inasema kinaga ubaga kuwa: َ“Hakika sisi tumeiteremsha Qur’an kwa lugha ya Kiarabu ili mpate kuifahamu”. Iwapo Qur’ani imeshuka kwa lugha ya kiarabu, ni lazima fani na fasihi ya lugha hii imetumika katika Qur’ani; na iwapo haya ni kweli, kwa nini tukatae kuwa katika Qurani mna majazi, istiara, na fani nyingine za balagha? Kwa kuwa Kiarabu hakiachani na fani hizi, kwa nini sisi tuzikatae fani hizi tunapofasiri Qur’ani? Suala la kuonekana ama kutoonekana kwa Mwenyezi Mungu huko Akhera limezuka kutokana na na matatizo mawili: Moja ni kutokuzichuja riwaya zilizosimuliwa juu ya maudhui hii, kwa kuzitazama sanadzake na matinizake ambapo Qur’ani ilitakiwa iwe ndio kipimo cha mwanzo cha kuzipima riwaya hizo. Pili ni tatizo hili tulilolitaja hapa la kutokwenda kwa mujibu wa fani za lugha ya Kiarabu. Kuzifasiri aya za Qur’ani bila ya kujali taratibu za asili ya lugha ya Kiarabu ni kupotosha Qur’ani yenyewe. 6 Surat Yusuf, aya ya 2. Katika kitabu hiki suala la kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na macho ya wanaadamu huko Akhera limepingwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa Qur’ani na Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Pia aya zilizotumiwa kama ni ushahidi wa kuthibitisha kuonekana kwa dhati ya Allah zimeelezwa na kufafanuliwa muradi wake na makusudio yake. Kwa kifupi aya zinazodaiwa na baadhi ya Waislamu kuwa zinathibitisha kuonekana kwa Mungu kwa macho huko Akhera unapozipeleka kwenye fani za lugha yenyewe, maana haya haitakubalika kwa vile zinapingana na aya nyingine kama utakavyoona hayo wewe mwenyewe. Kwa kuwa sisi Waislamu makimbilio yetu ni Qur’ani tukufu mjadala huu tumeuacha na kuukabidhi kwa Qur’ani ili tupate uamuzi sahihi. Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitachukuliwa kama ni chimbuko la kubadilishana mawazo tu wala si ushabiki na tusi kwa yeyote. Nitakuwa mwizi wa fadhila kama nitaacha kumshukuru ndugu yangu Sheikh Juma Mazrui wa Oman aliyetoa mawazo yake mengi kwangu katika kukamilisha Kitabu hiki kwa lengo la kuufikisha ujumbe huu wa Qur’ani Tukufu. Kwa hakika Sheikh Juma Mazrui amechukua bidii kubwa katika kuniongezea dondoo ambazo katika mazingira niliyokuwa nikiishi ilikuwa ni tabu sana kupata dondoo hizo, kuna uchache wa vitabu hapa nilipo, na wakati wa kutafiti kwangu ulikuwa mdogo kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika. Hakika namuomba Allah azidi kumpa Sheikh Juma Mazrui ufanisi na tawfiiq Duniani na Akhera ili aendelee kushirikina na waisilamu wenzake bila ya kujali rangi zao, kabila zao na madhehebu wanayofuata.Hakika sifa hii ya Sheikh Juma inapaswa kuigwa na kupigiwa mfano. Kama kulikuwa na malumbano ya kimadhehebu baina yangu na Sheikh Juma Mazrui miaka iliyopita ilikuwa amma ni kutokana na shetani au kutokana na nafsi zetu ambazo zilikuwa na hadi leo hii hazijakamilika, lakini nachukua nafasi hii kumlaani shetani na kumweka mbele Allah Subhanahu wataala kwa kila jambo, na namuomba Allah akijaalie Kitabu hiki kiwe ni sababu ya kuwaunganisha waisilamu wote Duniani, amin. Kwa hakika Sunni, Salafi, Shia na Ibadhi wote ni Waisilamu wanaohitajiana na inshaallah Kitabu hiki kitakuwa ndio ni moja ya funguo za fikra ya mlingano na kukurubiana na kuondoa tofauti kati ya waisilamu inshaallah. Ukamilifu wote ni wa Allah na kama kukiwa na kasoro yoyote kwenye kitabu hiki, kasoro hiyo inatoka kwangu natanguliza kuomba msamaha kwa kasoro hizo kwa Allah na kwa waisilamu wote.