Ni Nani Aliyeshinda Pale Karbala?
Ni Nani Aliyeshinda Pale Karbala?
0 Vote
309 View
Ni Nani Aliyeshinda Pale Karbala?
Katika vita vyote washiriki huwa wana malengo fulani ya kutimiza na kufaulu kunatolewa na kundi ambalo linafanikisha lile lengo lake na kushindwa hukasimiwa kwenye kundi ambalo hushindwa kulifikia lengo lake. Nini yalikuwa malengo ya Husein katika Vita vya Karbala na ni kwa kiwango gani amefanikiwa katika kulifikia lengo lake? Kitu gani Yazid alikuwa anapenda kukitimiza kwa kuingia katika vita na Husein? Je, yeye alifanikiwa katika kulifikia lengo lake?
Husein hakumpinga Yazid kwa sababu ya uadui binafsi kwake. Kama Husein angependelea tu kubakia hai katika ulimwengu au kama Yazid alikuwa tu angependa kwamba Husein akate mawasiliano yote na mambo ya kisiasa, hakuna haja ya vita kati ya watu hawa wawili ambayo ingeweza kutokea.
Kilichofanya vita kati yao viwe si yenye kuepukika ilikuwa kwamba baada ya yeye kufanya alazimike kuwa Khalifa juu ya Waislamu, Yazid pia alidai kuwa mrithi wa Mtume wa Uislamu. Katika kufanikiwa kwa lengo hili Yazid alimuona Husein kama ndio kipingamizi halisi, ingawaje Husein pengine angeepuka kula kiapo cha utii kwake katika hali ya kimya kimya.
Yazid alichochea kwa nguvu sana uhuishaji wa uyakinifu wa kipagani, lakini Husein alikuwa ngao ya kiroho na ibada ya Mwenyezi Mungu. Yazid alitenda na alisaidia uonevu na dhuluma, bali Husein alihusika na kudumisha ukweli na haki. Yazid alidhamiria kuziangamiza sheria na sifa pekee za Uislamu ambazo Husein aliiona kazi hiyo ni wajibu wake kuzidumisha na kuzilinda.
Ilikuwa ni kwa sababu hizi kwamba wakati akielezea nia yake katika kumpiga vita Husein, Yazid alidhihirisha msimamo wake wa kibeberu kwa kusema kwamba Husein amewafanya watu wajue haki zao, kwa hiyo, amehatarisha kuwepo kwa majumba mengi makubwa na makasiri makubwa, na kwamba ilibidi apigane na Husein ili kuulinda utawala wake na kusalimisha mali na utajiri wake.
Husein, kinyume chake, yeye alielezea mapambano yake dhidi ya Yazid kwa mashairi yenye maana; “Mwenyezi Mungu anatambua vyema kwamba chochote kile anachokimiliki Yazid hicho ni mali ya watu wengine kabisa. Alikuwa hana haki ya kukitwaa kwa matumizi yake binafsi. Kama, kwa kuwa mbadhilifu kama alivyo, angechagua kufanya uadilifu, angebadilisha njia zake (na mwenendo wake) na angetuliza fitina zake.”
Kama walivyo madhalimu wote, Yazid alilenga kupoozesha hisia za watu na kudumaza ari yao ya kuongea ukweli. Watu walikwishaacha kutumia akili zao katika kutafakari juu ya usawa wa madai ya mtawala wao juu ya madaraka. Hata kama kwa bahati isiyo ya kawaida mtu alifikiria kuhusu hilo, ujasiri wa mtu ulishindwa kutamka uamuzi ulio huru. Lengo la Husein lilikuwa kwamba uwezo wa hisia za watu ambao ulikuwa unafifia au kupungua nguvu na ujasiri wao wa kuzungumza waziwazi ambao ulikuwa umedhoofishwa, ni lazima vihuishwe na kudumishwa.
Katika mwaka wa 60 A.H. Waislamu mara kwa mara walishuhudia uovu na matendo ya karaha ya serikali ya Syria, lakini kwa ujumla walikuwa wamezidiwa na hali ya utepetevu na ukosefu wa hisia. Utokeaji wa ghafla wa tukio lisilo la kawaida ulihitajika kuwatikisa watu kutokana na uzito wao wa kiakili na kuziamsha hisia zao. Kifo cha kishahidi cha Husein kililitimiza hili kwa namna yenye athari kubwa. Mfano wake mtukufu uliwapa watu ujasiri wa (kuweza) kuelezea hisia zao.
Walipoona kwamba alikuwa sio Husein peke yake, bali sahaba zake wazee na vijana pia walijitoa muhanga kwa utulivu kamili, au waliposikia taarifa za tabia kama hizo, watu walikuja kukifikiria kifo kuwa chepesi zaidi kati- ka njia ya haki kuliko ambavyo wamewahi kukifikiria kabla ya hapo.
Kufanya jambo zaidi kupita kiasi mara nyingi huzaa matokeo ambayo ni kinyume cha vile ilivyokusudiwa. Yazid aliulundika uonevu juu ya uonevu dhidi ya Husein ili kwamba mwisho wake wa kusikitisha uwe kama onyo kwa wengine walioelekea kumpinga. Husein alikabiliana na ukatili wake wote kwa utulivu na subira, kiasi kwamba katika shauku yake ya ukatili, Yazid alishindwa kuutambua mpaka ambao kwamba watu labda wangeweza kuuvumilia uonevu, na ambao zaidi ya hapo hisia zao zilizolala, zenye ganzi zingeamshwa kwa nguvu kiasi cha kuufanya uonevu urudi nyuma na kujiangamiza wenyewe.
Al-Hurr bin Yazid al-Riyahii, afisa wa jeshi na baadhi ya watu katika jeshi la Yazid walijiunga na Husein katika siku ya mwezi 10 Muharram. Katika siku ya tatu baada ya mauaji ya Husein wakati Ubaydulah bin Ziyad alipoonyesha utovu wa adabu kwenye kichwa cha Husein, Zayd bin Arqam, sahaba mkongwe wa Mtume, alilalamika na kukipinga kitendo hiki. Wakati Yazid alipokirudia kitendo hiki cha Ibn Ziyad mjini Damascus cha utovu wa adabu mbaya sana kwenye kichwa cha Husein, sio tu Abu Barza al-Aslam bali hata balozi wa kikristo wa Mfalme wa Roma alimkosoa kwa ukali na uwazi kabisa.
Huu ulikuwa ndio ushindi wa Husein. Uongo (batili) ulikuja kupingwa wazi azi kabisa na kuchochea kutoafikiana kwa papo kwa hapo.
Kabla ya vita vya Karbala, nani angeweza kuwa na ujasiri kuongea habari za Husein kwa heshima kubwa mbele ya baraza laYazid? Baada ya watu wa Husein walioharibikiwa na kuporwa walipokwisha kufikishwa katika baraza yake kama wafungwa, Yazid ilimbidi asikilize kwa utulivu sifa nyingi zilizokuwa zikitolewa juu ya Husein.
Moja ya alama za uhakika kabisa ya kushindwa ni kwamba kundi lililoshindwa hujitoa kutoka kwenye msimamo lililokuwa limeuchukua kabla ya kuanza kwa mapigano. Kile ambacho kimesababisha vita kinaonekana kuwa kutowezekana kutimizwa. Vita kati ya Husein na Yazid vilikuwa vimeanzishwa kwa sababu Yazid alikuwa amesisitiza juu ya kupata kutoka kwa Husein kiapo cha utii kwake. Al-Husein alilikataa hili kwa uthabiti imara kabisa.
Je, Yazid alisimama imara kwenye dai lake hilo? Yazid alikuwa amependa kupata kiapo kutoka kwa Husein, siyo katika wadhifa wa Husein kama mtu tu wa kawaida, bali katika wadhifa wake kama mrithi wa kiroho wa Mtume. Baada ya kifo cha Husein, mtoto wake, Ali ibn Husein alichukua nafasi ile ile hasa kama baba yake. Ali ibn Husein na watu wote wa familia ya Husein waliosalimika baada ya vita vya Karbala walishushwa hadhi kufikia hali ya kuwa wafungwa. Kama Yazid asingesalimu amri kwenye suala la kiapo cha utii, angepaswa kulirudia dai lake kwa Ali ibn Husein. Hakuna kitu kama hicho ambacho kilipendekezwa kwake, kitu ambacho kinaonyesha wazi kwamba Yazid alikuwa amejitoa kwenye msimamo wake wa awali.
Matokeo yake, ni lazima ikubalike kwamba mwishoni, kati ya washindani hawa wawili, Husein aliibuka kuwa mshindi na Yazid kuwa ndiye aliyeshindwa.