UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S)
UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S)
0 Vote
262 View
UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S) Tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu wa Kishia na Waislamu wa Kisunni ni juu ya imani ya Ukhalifa na Uimamu baada ya kuondoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SA.W.W). Sisi waislamu wa Kishia tunaamini kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni khalifa na ni Imam wa kwanza baada ya Mtume (S.A.W.W) ambapo ndugu zetu Waislamu wa Kisunni wanaamini kwamba Seyidina Abubakar ( r.a.) alikuwa ni khalifa wa kwanza. Ingawa kuna tofauti nyingine ndogo ndogo zilizopo baina ya madhehebu makubwa ya Uislamu (Shia na Sunni) kwa mfano katika sheria (Fiqh) kama vile kukunja mikono wakati wa kusali au kuinyoosha n.k. lakini hizi ni tofauti ndogo ndogo sana ambazo zinaweza hata kupatikana ndani ya madhehebu manne ya Kisunni (Imam Shafi, Maliki, Hanafi na Hanbali ). WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI UKHALIFA WA IMAMU ALI (A.S) Tofauti kubwa iliyopo baina ya Waislamu wa Kishia na Waislamu wa Kisunni ni juu ya imani ya Ukhalifa na Uimamu baada ya kuondoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SA.W.W). Sisi waislamu wa Kishia tunaamini kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni khalifa na ni Imam wa kwanza baada ya Mtume (S.A.W.W) ambapo ndugu zetu Waislamu wa Kisunni wanaamini kwamba Seyidina Abubakar ( r.a.) alikuwa ni khalifa wa kwanza. Ingawa kuna tofauti nyingine ndogo ndogo zilizopo baina ya madhehebu makubwa ya Uislamu (Shia na Sunni) kwa mfano katika sheria (Fiqh) kama vile kukunja mikono wakati wa kusali au kuinyoosha n.k. lakini hizi ni tofauti ndogo ndogo sana ambazo zinaweza hata kupatikana ndani ya madhehebu manne ya Kisunni (Imam Shafi, Maliki, Hanafi na Hanbali ). Masuala haya tutayajadili hapo baadae InshaaAllah. Mbali na tofauti hiyo kubwa, kuna mambo yanayofanana katika imani za Waislamu wa Shia Ithnaa Ashariyya na Waislamu wa Kisunni. La kwanza ni nguzo tano za Uislamu, yaani : (a) Shahaada - Laa Ilaaha Illallah - Muhammadur Rasuulullah - Hakuna Mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah - na Muhammad ni Mtume wa mwisho wa Allah. (b) Sala tano za kila siku (c) Kufunga mwezi wa Ramadhan (d) Kuhiji katika nyumba takatifu ya Kaa'ba (e) kutoa Zaka kwa ajili ya maskini. Kwa pamoja Shia Ithnaa Asheriyya na Sunni wanaamini kua kitabu cha mwisho cha Allah Qur'an bado kipo vile vile bila mapunguzo au maongezo, na wanajaribu kufuata maamrisho yake bila kubakisha kitu. Kwa pamoja Shia Ithna Asheriya na Sunni wanaichukulia Sunnah na Sira (namna alivyoishi Mtume s.a.w.w) ya Mtume kuwa ni muongozo kwa Waislamu katika maisha yao ya kila siku na wanajaribu kuifuata kwa uangalifu mkubwa ili wapate kuokoka hapa duniani na Akhera. Ingawa wapo watu waharibifu katika jamii ambao kwa kuto kua na elimu tosha, wanatushutumu sisi Shia Ithna Asheriya kwa madai mbalimbali ya uongo kama vile kudai kua Shia wana Qur'an yao au madai kua eti Shia wanaamini kua Utume ulikua ni wa Imam Ali bin Abitalib, n.k. Wale wote wanaoutafuta ukweli, wanatakiwa kuyatupilia mbali madai (shutuma) haya maovu dhidi yetu na tunawaomba watembelee misikiti na madrasa zetu ambazo mara zote zipo wazi kwa Muislamu yeyote kuja kuthibitisha imani zetu. Kuna Shia zaidi ya millioni 250 duniani kote ambao wanaamini kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni Mtume wa mwisho na wanafuata maamrisho ya Qur'an na Sunna za Mtume (S.A.W.W) katika maisha yao ya kila siku. Katika manispaa ya Dodoma peke yake, sisi Shia tuna misikiti miwili; Khoja Shia Masjid na Masjid Imam Mahdi (A.S) na tunawaalika waumini wote wa Kiislamu kututembelea katika misikiti hii ili kupata ushahidi kwa macho yao kuhusiana na imani na matendo yetu kabla ya kuangukia katika mtego wa waharibifu wanaotuzulia habari za uongo.