KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

Publish number :

Toleo la kwanza

Publish location :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho From Marriage to Parenthood. Sisi tumekiita, Kuanzia Ndoa Hadi Kuwa Wazazi. Kitabu hiki kinazungumzia masuala yote yanayohusu wanandoa: kuanzia kufunga kwao ndoa - waishi vipi, mpaka watakapopata watoto - wawalee vipi - kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Kama ambavyo inafahamika kwamba Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha, basi kwa hakika haukuacha hata kitu kimoja kinachohusu maisha ya mwanadamu, pamoja na kumhudumia kiroho. Ndoa ni taasisi ambayo iliasisiwa na Allah ‘Azza wa Jallah Mwenyewe pale alipowaunganisha baba yetu Adam na mama yetu Hawa kuishi pamoja kama mume na mke. Kwa hiyo, Uislamu kama dini na mfumo wa maisha, umeweka kanuni, sheria na hukumu za kufuatwa ndani ya taasisi hii tukufu (ya ndoa). Waandishi wa kitabu hiki wamefanya juhudi kubwa ya kukusanya mafundisho yote muhimu yenye kuhusu taasisi hii kutoka katika vyanzo vikubwa na chimbuko la sheria na mafundisho ya Uislamu, ambavyo ni Qur’ani na Sunna Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.