Swala ni Nguzo ya Dini

Swala ni Nguzo ya Dini

Swala ni Nguzo ya Dini

Interpreter :

Ibrahim Khamisi

Publish number :

Toleo la kwanza

Publish location :

Dar-es-Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Swala ni Nguzo ya Dini

Kitabu kilichoko mikononi mwako ambacho ndani yake Sala (swala) imeelezwa pamoja na vielelezo vya picha, tumekiita: Sala ni Nguzo ya Dini. Sala ni nguzo kubwa ya dini. Mtukufu Mtume (s.a.w.) amesema: "Sala ni nguzo ya dini, mwenye kuivunja ameivunja dini, na mwenye kuisimamisha ameisimamisha dini." Mtukufu Mtume ameongeza: "Kila kitu kina uso, na uso wa Uislamu ni Sala. Mwenye kuacha kusali ameuchafua uso wa dini." Imam Muhammad Baqir (a.s.) amemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.) akisema: "Kitu cha kwanza atakachohesabiwa muumini (Siku ya Kiyama) ni Sala. Ikikubaliwa yatakubaliwa matendo mengine, na ikikataliwa yatakataliwa matendo mengine pia." Kwa ufupi, kuna hadithi nyingi sana kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) na Maimamu (a.s.) kuhusu umuhimu wa Sala kiasi kwamba katika hadithi moja, Mtukufu Mtume (s.a.w.) amesema kwamba kitu chenye kutofautisha baina ya Uislamu na ukafiri ni sala. Wakati huu tulionao una mitihani mingi sana, vijana wa Kiislamu na wazee pia wamejitumbukiza katika vitendo viovu na vichafu kiasi kwamba mtu hawezi kumtofautisha na mnyama, na pengine hata mnyama ni afadhali. Ili kuishinda mitihani hii na maovu haya, dawa yake ni kushikamana na sala. Allah 'Azza wa Jalla anasema katika Qur'ani Tukufu: "… Hakika Sala huzuia mambo machafu na maovu, na kwa hakika kumbuko la Allah ni (jambo) kubwa kabisa, na Allah anajua mnayoyatenda." (29:45) Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan katika wakati huu ambapo jamii inazidi kudidimia katika maovu kutokana na kumomonyoka kwa maadili mema. Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Mustafa Ranjbar Shirazi, na ndugu yetu Ibrahim Khamisi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha uchapishaji wa kitabu hiki.