ADABU ZA SOKONI NA NJIANI

ADABU ZA SOKONI  NA NJIANI

ADABU ZA SOKONI NA NJIANI

Interpreter :

Amiri Mussa Kea

Number of volumes :

1000

Publish location :

S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

ADABU ZA SOKONI NA NJIANI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Aadaabu ‘s-Sawq wa ‘t-Tariiq. Sisi tumekiita, Adabu za Sokoni na Njiani.Kitabu hiki kimeandikwa na Jumuia ya Maarifa na Utamaduni wa Kiislamu. Inafahamika vizuri kwamba kwa vile Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha, hivyo, haukuacha jambo lolote linahusu maisha ya mwanadamu. Uislamu umetengeneza kanuni, sheria na adabu zinazohusu kila suala la mwanadamu. Soko na njia ni maeneo ambayo watu wa kila aina huyatu-mia katika maisha yao ya kila siku. Katika muktadha huu, soko ni kuanzia maduka madogo ya mitaani, maduka makubwa (supermarkets),na masoko ya kitaifa na kimataifa. Njia katika muktadha huu ni kuanzia njia za kawai-da wanazotumia watu (za miguu), barabara za magari, reli, usafiri wa maji-ni na angani, kitaifa na kimataifa. Kwa hiyo, Uislamu umeweka kanuni, sheria na adabu kwa ajili ya matumizi ya watu katika maeneo hayo ili kulinda haki ya kila mtu. Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kanuni, sheria na adabu zinazotumi-ka katika maeneo hayo kwa mujibu wa mafundisho ya Kiiislamu ambayo ni kutoka katika Qur’ani Tukufu na Sunna. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, kwani kinagusa harakati za maisha ya watu ya kila siku. Tunakitoa kwa lugha ya Kiswahili kwa malengo yetu yaleyale ya kuwahudumia wasomaji wetu wazungumzaji wa Kiswahili ili wapate kuongeza elimu yao ya dini na ya kijamii kwa ujum-la. Adabu za sokoni. By Lubumba.qxd 6/22/2009 8:54 AM Page F Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Amir Musa Kea kwa kukubali kukitar-jumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.