ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE (ASLU’SH-SHIA WA USULUHA)

ASILI YA USHIA NA  MISINGI YAKE (ASLU’SH-SHIA WA USULUHA)

ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE (ASLU’SH-SHIA WA USULUHA)

Publication year :

2005

Number of volumes :

1

Publish number :

Toleo la kwanza

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE (ASLU’SH-SHIA WA USULUHA)

Katika uandishi uliojaa utata, mara nyingi hudaiwa kwamba Madhehebu ya Sunni ni “Imani Sahihi” ya Kiislamu na kwamba madhehebu ya Shia ni “Madhehebu iliyozushwa”, na ni madhehebu iliyoanzishwa kwa lengo la kufanya mapinduzi ndani ya Uislamu. Wazo hili wakati mwingine huelezwa kwamba “Ushia” ulianza kamaharakati za kisiasa na baadaye kupata nguvu ya kidini. Huu upinzani dhidi ya Ushia, haukomi tu kwa Waandishi wa karne zilizopita, bali hata Wanazuoni wa Kisunni wa karne hiiwanakubaliana na mawazo haya. Wanazuoni kama Abul Hassan Ali Nadwi, Manzur Ahmad Nu’mani (wote wawili wa India), Ihsa’n Illahi Zahir (wa Pakistan), Muhibbu ‘d-Din al-Khatib na Mussa Ja’r Allah(wa Mashariki ya Kati); wanaunga mkono mawazo haya. Nadharia hii inakubaliwa pia na kikundi cha Wanazuoni waliohitimu kutoka Seminari za Kidini na ambao hawakusoma kabisa Elimu Dunia.Fazlur Rahman (wa Pakistan) na Ahmad Amin (wa Misri) wamo katika kundi hili. Kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluha kiliandikwa ili kujibu maandishi ya Ahmad Amin aliyoyaandika katika kitabu chake Fajru’l-Islam. Mwandishi mashuhuri wa kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluha ni al-‘Allamah ash-Sheikh Muhammad al-Husayn Al-e Kashiful-Ghita (alifariki 1373 A.H.) ambaye alikuwa mmoja wa Mujtahid mashuhuri wa karne iliyopita, kwa mukhtasari ameelezea Imani na matendo ya ibada ya madhehebu ya Shia na halikadhalika michango ya Shia (miongoni mwa masahaba na tabi’in) katika nyanja mbali mbali za Sayansi ya Dini katika Uislamu. Katika kitabu hiki amejadili pia mada kama vile raj’at, ‘Abdulla’h bin Saba’, bada’a, na taqiya. Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ya Aslu’sh-Shia wa Usuluha ilitafsiriwa na Sheikh Muhammad Nasser (aliyeukubali Ushia hivi karibuni) katika mwaka wa sitini na nane. Marehemu baba yangu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alipelekea Mswa’da wa Tafsiri hiyo kwa Bw. Ibrahim Qassim wa Zanzibar na Agha Sayyid Muhammad Mahdi Shushtari kwa ajili ya kuhaririwa. Wote wawili kwa pamoja walihariri nusu ya Mswa’da huu, na nusu iliyobakia ilihaririwa baadaye na Agha Sayyid Mahdi. Marehemu Agha Mahdi alipohamia Tehran, alianza kutafsiri upya Aslu’sh-Shia wa Usuluha na ilichapishwa kwa mtiririko katika matoleo ya Gazeti la Sauti ya Umma chini ya jina “Asili ya Shi’a” iliyotafsiriwa na Agha Mahdi. Hata hivyo, hiyo haikuwa tafsiri ya kitabu kamili. Marehemu baba yangu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alipotembelea Iran mwaka 2000, kwa ajili ya matibabu ya moyo, katika kikao chake na Ayatullah Sayyid Ali al-Khamenai, Kiongozi huyu mtukufu alionyesha shauku yake ya kuona kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluha katika lugha ya Kiswahili. Baada ya kuipitia sehemu ya tafsiri iliyokuwa tayari wakati huo, Marehemu Baba alimwambia Sheikh Musabbah Shaban kufasiri upya kwa lugha ya Kiswahili kutoka kwenye toleo la lugha ya Kiarabu kilichochapishwa na “Imam Ali Foundation (Qum)”, yenye rejea fasaha kilichoandikwa na Bw. Alla Al-e-Ja’far, mwaka 1415 A. H.Unayoiona mikononi mwako ni ile tafsiri mpya. Tunamuomba Allah (s.w.t.) ateremshe Rehema Zake juu ya Roho za Mwandishi, Wafasiri wa mwanzo na Wahariri wote. Pia tunamuomba Allah (s.w.t.) amlipe Sheikh Musabbah kwa kazi hii na amzidishie Tawfeeq aweze kutangaza na kueneza mafundisho ya Uislamu wa kweli miongoni mwa Jamii zizungumzao lugha ya Kiswahili.