BWANA ABU TALIB [A]

BWANA ABU TALIB [A]

BWANA ABU TALIB [A]

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

BWANA ABU TALIB [A]

Bismilahir Rahmanir Rahiim Alhamdu li waliyyihi was-Salaatu-ala Nabiyyihi wa Aalihil Aimmati wa Awliyail Ummah. Kitabu hiki kiitwacho Bwana Abu Tallb [a] madhulumu wa historia ni tarjuma ya juzuu ya 7 na 8 ya kitabu mashuhuri kiitwacho AI-Ghadiir cha Allamah al-Amini na ambacho kinazungumzia hali ya maisha ya Bwana Abu Talib [a] ambaye ni baba mzazi wa Amir al-Mu'miniin Imam Ali ibn Abi Talib [a]. Kama vile zilivyofanywa kazi zigine za utafiti basi mtunzi wa kitabu hiki cha Al-Ghadiir ametimiza wajibu wake pia. Katika lugha nyingi sana kumeandikwa kwa uchache sana kuhusu Bwana Abu Talib [a] na hayo machache yaliyoandikwa kuna mambo mengi mno yenye kutatanisha ndani yake. Mazungumzo makubwa sana katika maisha yake ni kule kuangalia na kutafakari Bwana Abu Talib [a] amefanya mambo gani na ameyafanyaje mambo hayo katika umri wake huo kwa mujibu wa ushahidi wa kihistoria ambayo machache yake yamo katika kitabu hiki-tunaona kuwa Bwana Abu Talib [a] wakati wake mwingi ameutumikia Uislamu na vile vile katika kumhifadhi na kumnusuru Mtume [s]. Katika hali hii yeye ameweza kuvumilia hasira na ukali wa chuki za kabila lake la Maquraish kiasi cha yeye na hao wachache walipokuwa wametolewa nje ya mji wakakaa katika Shayb-i-Abu Talib na wakastahimili matatizo na dhiki zote na wakaweza kufanya subira ya hali ya juu. Kwa hakika ni kwamba wakati huo ndio uliokuwa wa harakati na mikakati mipya ya mapinduzi ya Kiislam ambayo yalikuwa yakitekelezwa na Mtume [s]. Kwa hakika Shayb-i-Abu Talib kisa chake hicho kinaonyesha wazi uhalifu uliokuwa ukifanywa na Maquraish kisiasa kiuchumi na kimaisha na kijamii vilevile cihidi ya Mtume [s] na watu wake. Katika hali ngumu kabisa kama hizi na zinginezo tulizonazo katika historia Bwana Abu Talib kwa nyakati mbalimbali ameweza kujitolea yeye mwenyewe kumnusuru na kumlinda Mtume [s] na vile vile amewaamrisha wanawe Ali [a] na Jaafer [a] wawe daima wakijitolea kwa ajili ya kumnusuru na kumwokoa Mtume [s]. Kwa mukhtasari kabisa tunaona kuwa maisha yake yote alikuwa ameshajitolea katika kuunusuru na kueneza Uislamu na kumwokoa na kumkinga Mtume [s] kwa sababu tu yeye alikuwa amekwishaongoka na kupata hidaya ya Islam. Yeye wakati wa mwisho wa pumzi yake alikuwa akiwasisitiza na kuwahimiza watoto na jamaa zake wawe daima mbele katika kumnusuru na kumkinga na kumuunga mkono Mtume Muhammad [s] katika kueneza Uislamu. Na vile vile kwa kifo chake (ambacho kilikuwa baada ya kifo cha Bi Khadijat-il-Kubra) Mtume [s] alikuwa amehuzunika mno kiasi kwamba alikuwa ameutangaza mwaka huo kuwa ni aamul huzun yaani mwaka wa huzuni kubwa. Kwa kupata mwangaza huo bado tunaona katika vitabu vingine vya kihistoria vya madhehebu mengine yakiwa yanamtaja Bwana Abu Talib kuwa ni mushrik na kuthubutu kumsema kuwa ni kafiri. Kwa hakika tuhuma kama hizi katika historia ni njama kubwa sana zilizofanywa na wamejaaribu hao waliotoa tuhuma hizo kuthibitisha tuhuma zao kwa aya za Qurani tukufu na hadithi za Mtume [s]. Kama tutakavyoweza kuona vyema madhumuni makubwa ya hawa watoao tuhuma kwa kusema Bwana Abu Talib ni mushrik na kafiri huku wakimchukulia yeye kuwa ni mtu mmoja wa kawaida lakini siri ya malengo yao ni kule kuthibitisha kuwa baba yake Imam Ali ibn Abi Talib [a] alikuwa ni mushriki na kafiri ili waweze kumvunja nguvu Imam Ali [a]. Ni dhahiri kuwa ni jambo ambalo tunalielewa kuwa iwapo baba atapata pigo basi shida hiyo kubwa itamfikia na kumwathiri mtoto wake katika maisha na nyadhifa zake. Lakini kama tulivyokwisha kuona kuwa malengo yao sio Bwana Abu Talib mwenyewe bali wao wanataka kumdhoofisha na kumvunja nguvu Imam Ali [a] kuwa baba yake alikuwa hana imani na alikuwa mushriki na kafiri ili kwamba Imam Ali [a] hali na maisha yake yawe na dosari kubwa. Vyote tulivyokwisha kuvisoma hapo juu, usahihi wake au uwazi wake unakuwa pale wakati tunapoona kuwa historia hii hii na waandishi hawa hawa na wanonakili riwaya hawa hawa ambao wanatoa uamuzi kama huo kuhusu Abu Talib [a] - wanakaa kimya kuhusu wazazi wao waliokuwa wakija daima mbele ya Imam Ali [a] katika maisha yao - wao daima wamekuwa wakiyeyuka mbele ya nuru ya Imam Ali [a] kwa kutoweza kustahimili nuru hiyo. Tunaona kuwa waandishi hawa hawa na wanaoripoti riwaya hizi ndio wanaoandika fadhila zake lakini tunashangaa kuona pamoja na kuandika sifa na fadhila na daraja zake makabila yao na watu wao wanashindwa kupambanua upotofu huu ulivyo ndipo hapo tunaona kuwa Allamah Amin amefanya utafiti wa hali ya juu usio na kifani na ameweza kuchambua historia kwa undani kabisa pamoja na matukio na riwaya na ametupatia matunda mazuri mno ya kazi yake ambayo imejibu na imeweza kuondoa tuhuma zote dhidi ya Bwana Abu Talib [a] kuwa yeye alikuwa ni mushrik na kafiri. Bwana Amini ameweka uwanja wazi kama tutakavyoweza kushuhudia wenyewe kuwa Bwana Abu Talib kamwe hakuwa mushrik wala kafiri. Hata hivyo inabidi kitabu kijiarifishe chenyewe hivyo sisi tunayafupisha mazungumzo haya ili msomaji aweze aweze kujibwaga katika uwanja wa utafiti ili kufikia majibu na kuwapima viongozi wanaotoa tuhuma dhidi ya Bwana Abu Talib [a].