FATIMA Al-ZAHRA

FATIMA Al-ZAHRA

FATIMA Al-ZAHRA

Publication year :

2008

Publish number :

la kwanza

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

FATIMA Al-ZAHRA

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Fatimah al-Zahra.Sisi pia tumekiita, Fatima al-Zahra. Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatima Zahra (a.s), binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kati ya mihadhara ya thamani ya mare-hemu Imam Muhammad al-Husaini al-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehe-mu). Ni kitabu cha aina yake katika lugha ya Kiswahili kinachoelezea maisha ya Bibi huyu mtukufu mwenye nuru. Cha kuzingatia ni kwamba kumjua mtukufu huyu ambaye ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ni wajibu kwa Waislamu wote, kwani ameshasema: “Jueni kwamba mimi ni Fatima al-Zahra.” Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini. Bibi Fatima (a.s.) ni maasumu wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na kumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul Muuminina Ali (a.s) na watoto wake walio maasumu (a.s). Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 5/25/2009 8:27 AM Page D Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali juku-mu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.