HADITHI YA THAQALAINI KATIKA VITABU VYA AHLI SUNNA
HADITHI YA THAQALAINI KATIKA VITABU VYA AHLI SUNNA
Interpreter :
Number of volumes :
1000
Publish number :
Toleo la kwanza
Publish location :
Dar es Salaam, Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
HADITHI YA THAQALAINI KATIKA VITABU VYA AHLI SUNNA
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Hadith ath-Thaqalaynkilichoandikwa na Dk. Sayyid Alaauddin al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwini. Sisi tumekiita, Hadithi ya Thaqalain. Kitabu hiki, Hadith ya Thaqalainni hadithi maarufu sana katika ulimwen-gu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayohaikutaja hadithi hii, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kuitaja hadithi hii. Hadithi ya Thaqalain ni wasia ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.) alioutoa kwa Waislamu pale Ghadir Khum wakati anarudi kutoka kwenye Hija yake ya mwisho (maarufu kama Hijjatu ’l-Widaa). Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir Khum ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.) alitoa khutba ndefu ambayo kwayo alitoa kauli hii inayo-julikana kama hadithi ya Thaqalain: “...Ninakuachieni vizito viwili (thaqalayn);Qur’ani Tukufu na Kizazi changu...” Baada ya tukio hili la Ghadir, aya ifuatayo iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.): “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nime wapendeleeni Uislamu uwe dini yenu...”(5:3) Baada ya kushuka aya hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alimwita Ali juu ya mimbari ambayo ilitengenezwa kwa matandiko ya ngamia, kisha akanyun-yua mkono wake akasema: “Man kuntu mawlahu fahadha Aliyyun mawlahu.”(Yule ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake basi huyu Ali (naye) ni mwenye kutawalia mambo yake.” Kisha akaomba dua: “Ewe Allah! Msaidie mwenye kumsaidia (Ali) na mpige vita mwenye kumpiga vita (Ali).” (Rejea ya hadithi hii utaipata kwenye kitabu hiki kadiri unavyoendelea kusoma) Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Amir Musa kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.