KWA NINI MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) ALIOA WAKE WENGI?
KWA NINI MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) ALIOA WAKE WENGI?
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2001
Number of volumes :
2000
Publish number :
Toleo la Nne
Publish location :
Dar es Salaam, Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
KWA NINI MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) ALIOA WAKE WENGI?
Mwanzoni mwa karne ya kumi na nane waandishi wa Kikristo waligundua mbinu mpya za kuushambulia Uislamu. Nia yao ilikuwa ni kuyaeneza maandishi yasiyo na ukweli ili kupotosha watu kutoka katika lengo na msingi mathubuti wa Kiislamu na kuitweza heshima ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.). Kiini cha uzushi huo kilikuwa ni vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa Kikristo wa karne ya kumi na tano. Mwandishi moja aliwahi kuandika kitabu kiitwacho “Refutation to the Religion of Muhammad (Kuikanusha Dini ya Muhammad)”, ambacho ndio msingi wa waandishi wengine waliofuata katika kuipinga dini ya Kiislamu. Waandishi hawa, hawakujua ukweli wa mambo kuhusu Uislamu kwa sababu walikuwa hawana ujuzi wa lugha ya Kiarabu, na hali vitabu vya historia ya Kiislamu na Vitabu Vitakatifu vilivyopatikana katika zama hizo viliandikwa kwa Kiarabu. Kwa hiyo, haikuwa ajabu kwa Waandishi hao kuandika maandishi ya kumpinga Mtume wa Uislamu na kumuambia kuwa alikuwa na tamaa ya wanawake kwa sababu ati alioa wanawake wengi ambapo Waislamu wengine waliruhusiwa kuoa wanawake wanne tu. (Waandishi hao walisahau kwamba waandishi wa Biblia la siku hizi wamewashtaki Manabii wao kwa kuwa na tamaa ya zinaa!). Hakika, kwa kutowaeleza ukweli ndugu zao Wakristo, na kumsingizia Mtume wa Islamu (s.a.w.w.) waandishi hao walitumainia mkuyasimamisha maendeleo ya haraka ya kuenea kwa dini ya Kiislamu. Lakini mbinu hizi hazikusaidia vizuri. Tunawaona wanachuoni wa Kikristo wenye busara wakimtetea Mtume (s.a.w.w.) dhidi ya masingizio hayo kwa kuyahanusha. Bila shaka hadithi hizi za masingizio kwa mtume (s.a.w.w.) hazikubaliwi hata kidogo na Waislamu, kwa sababu sehemu ya imani yao ni kuiamini “Ismat” (Utakatifu au kutokosea) ya Mitume (s.a.w.w.). Wakatii huo huo ni muhimu (kwetu sisi Waislamu) uwafahamisha wale wasio Waislamu ukweli wa mambo.