UTOKEZO (AL-BADAA)
UTOKEZO (AL-BADAA)
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2009
Number of volumes :
1000
Publish number :
Toleo la kwanza
Publish location :
Dar es Salaam, Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
UTOKEZO (AL-BADAA)
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, al-Badaa’.Sisi tumekiita, Utokezo. Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni wa Kiislamu, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani. Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususan miongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ - yaani utokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanase-ma kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi ya wanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamu wenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina au makafiri. Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili kati-ka dini kama utakavyoona katika kitabu hiki. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imea-mua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul-Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.