UTUMWA – MTAZAMO WA KIISILAMU NA WA (NCHI ZA ULAYA) MAGHARIBI.

UTUMWA – MTAZAMO WA KIISILAMU NA WA (NCHI ZA ULAYA) MAGHARIBI.

UTUMWA – MTAZAMO WA KIISILAMU NA WA (NCHI ZA ULAYA) MAGHARIBI.

Publish number :

Toleo la kwanza

Publish location :

Dar-es-Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

UTUMWA – MTAZAMO WA KIISILAMU NA WA (NCHI ZA ULAYA) MAGHARIBI.

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la “Slavery – Islamic & Western Perspectives kilichoandikwa na Mwanachuoni mkubwa Marhum Allamah Sayyid Sa’eed Akhtar Rizvi. Kitabu hiki kwa ufupi kinaelezea juu ya biashara ya utumwa ilivyokuwa ikiendeshwa na wazungu hapa Afrika, wakisaidiwa na Kanisa Katoloki na Makinisa mengine yaliyofuatia. Mwandishi kwa kutumia elimu, akili, mantiki na utafiti wa kina, amefichua ukweli wote uliokuwa umejificha nyuma ya biashara hii ya udhalilishaji wa binadamu. Hapa Afrika na duniani kote, watu wangali wanaamini kwamba biashara ya utumwa hapa Afrika (hususan Afrika ya Mashariki) ilianzishwa na kuendeshwa na Waraabu wakiungwa mkono na Uislamu. Kwa hiyo mbele za watu Uislamu ulionekana kama dini isiyojali ubinadamu, iliyowaswaga mababu zetu kama wanyama na kuwafanya watumwa kwenye nchi zao. Mwandishi anayakanusha yote haya, na kuonyesha jinsi gani Uislamu ulivyokuwa dhidi ya biashara hii ya tumwa, na ulivyofanya ili kukomesha biashara hii. Na kuonyesha jinsi gani Wazungu walivyoing’ang’ania biashara hii, na jinsi Mapadre na Maaskofu walivyozibariki meli zilizokuwa zimebeba watumwa. Tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu (na wasio kuwa Waislamu) wazungumzaji wa Kiswahili, na hili likiwa ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya ‘Al`Itrah Foundation’ katika kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akh Salman Shou kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu, na kuondokana na dhana hii potofu juu ya biashara ya utumwa.