FADAK

FADAK

FADAK

Interpreter :

Mohammad Said Kanju

Publication year :

2004

Number of volumes :

2000

Publish number :

1

Publish location :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

FADAK

DIBAJI Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Watukufu Ahlul~Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki “Fadak”. Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya maandishi vya Marhum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.). Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Ki-Islamu na kilitafsiriwa na kuchapishwa na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Ki-Urdu, Ki-Hindi na Ki-Gujrati. Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama ile za mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya watu wengi kutoka Afrika ya Mashriki kutaka kujua kadhia ya muhimu na ya maana sana katika historia ya Uislamu, kadhia ya Fadak. Hii ilitufanya tutafsiri na kuchapish kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili ili watu wazungumzao kiswahili wa weze kuelewa na kufahamu dhuluma na maonevu yaliyotendwa kwa Ahlul Bayt (a.s.) watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.). Mimi binafsi sikusita kumuomba ndugu yetu Dr Muhammad Kanju kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya lugha ya Kiingereza, Namshukuru Dr Kanju kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja. Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi mwao na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu za Tabligh.Tunamuomba Allah (s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko, Akhera.