Abdallah ibn Saba na ngano nyingine

Abdallah ibn Saba na ngano nyingine

Abdallah ibn Saba na ngano nyingine

Publication year :

2004

Publish location :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Abdallah ibn Saba na ngano nyingine

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la"Ibn Saba and other myths" (Ibn Saba na ngano nyingine) kilichoandikwa na Sayyid Murtadha Al - Askari Kitabu hiki kimeandikwa na Mwanachuoni mkubwa, mwanahistoria na mtafiti. Kitabu hiki kinahusu ngano ya Ibn Saba mtu ambaye hajawahi kuishi katika ulimwengu huu. Lakini mtu huyu ambaye amepachikwa jina la Abdullah Ibn Saba, amesukwa kwa maneno katika vitabu vya historia mpaka watu wakaamini kwamba kweli alikuwepo mtu kama huyu, na baya zaidi, watu wakapotoshwa kwamba huyu ndiye aliyeanzisha Ushia. Ili kuwatoa watu katika dhana hii potofu Mwanachuoni huyu mahiri amefanya utafiti wa kina na kuthibitisha pasina shaka yoyote kwamba hajakuwepo mtu kama huyu duniani. [Itabidi wale wanaoshikilia dhana hii, kama hawataki ukweli, wamtafute Ibn Saba mwingine lakini sio huyu tena]. Kutokana na ukweli huu tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili ili kuondokana na dhana hii potofu. Na hili ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' katika kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akhy Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.