YAZID HAKUWA AMIRUL-MU’MININ
YAZID HAKUWA AMIRUL-MU’MININ
(0 Kura)
(0 Kura)
YAZID HAKUWA AMIRUL-MU’MININ
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu; na swala na salamu zimshukie Mtume Wake pamoja na aali zake waliotwahirishwa; amin. Mwanzo mwanzo wa mwezi wa Muharram wa mwaka huu (1424 BH), palitolewa karatasi katika mji wa Mombasa zenye kichwa cha habari “Barua ya wazi kwa wahubiri na maimamu wa sunna” (uk. 30 humu). Lengo la karatasi hizo lilikuwa ni kuwaonyesha hao wahubiri na maimamu wa kisunni makosa wanayoyafanya ya kuweka “vikao vya mawaidha, khususan katika siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharram”. Kwa maoni ya waandishi wa karatasi hizo, “hakuna hadith (dalili) ambayo inatuambia tufanye hivyo” isipokuwa huo ni “uzushi” ambao, kwa kuufanya, “mwawapoteza wafuasi wa Sunna kwa kuwaiga hao hao Ma-Shia”. Waliozitoa karatasi hizo walijiita “Ahlul-Tawheed” ambao, kama wasomi wote wanavyojua, ni mawahabi. Wao hutumia jina hilo kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza ni kuficha uwahabi wao wanaojua kwamba unapingwa na Waislamu wote. Kwa hivyo wanaogopa kukosa kuungwa mkono. Sababu ya pili ni kutokana na ile imani yao kwamba wao peke yaondio wanaompwekesha Mwenyezi Mungu; Waislamu wengine wote wasiokubaliana nao, kwao wao, ni mushrikina. Lakini kwa kuwa Waislamu wotewanaamini kwamba wao ni ahlut tawhiid, kwa vile wotewanaikiri Laa ilaaha illallaah, waandishi wa karatasi hizo, kwa kutumia jina hilo, walitaka kuwavungavunga Waislamu wawafikirie kuwa ni wenzao. Ili kuzijibu tuhuma walizozifanya dhidi ya mashia kuhusu mauaji ya Imam Hussein (a.s.), na ili kuyasahihisha madai waliyoyafanya katika karatasi zao, kuwa Yazid alikuwa Amirul-Mu’minin, nilitoa mfululizo wa karatasi kumi, kuanzia tarehe 8 Muharram 1424 / 12 Machi 2003 hadi 14 Rabii-ul-Awwal 1424 / 16 Mei 2003, nilizozipa kichwa cha habari “Barua ya wazi kwa mawahabi.” Karatasi hizo ndizo hizi tulizozikusanya katika kitabu hiki. Na kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu.