Drawer trigger

Asili ya Madhehebu katika Uislamu

Asili ya Madhehebu katika Uislamu

Asili ya Madhehebu katika Uislamu

Publication year :

2010

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Votes)

QRCode

(0 Votes)

Asili ya Madhehebu katika Uislamu

Kitabu kilichoko mikononi mwako kinaitwa, Asili ya Madhehebu katika Uislamu, kilichoandikwa na Ndugu Isa Rwechungura kwa lugha ya Kiswahili. Maudhui kubwa katika kitabu hiki ni kuhusu madhehebu za Kiislamu. Suala la madhehebu limekuwa na bado halieleweki vizuri miongoni mwa Waislamu kiasi kwamba wakati mwingine hufikia kupigana na kuuana kutokana na kuzozana juu ya suala hili. Suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAW mwenyewe katika hadithi zake tukufu: “Mayahudi walikuwa madhehebu sabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini na mbili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehebu sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) Motoni isipokuwa moja.” Kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba suala la madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo bali changamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zote hizo zitaingia Motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafiti ili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama, na sio kugombana kwa jambo ambalo lilikwishatabiriwa na Bwana Mtume mwenyewe  na hiki ndicho alichofanya mwandishi wa kitabu hiki. Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Shukurani zimuendee mwandishi wa kitabu hiki, tunamwomba Allah Mwenye uhai wa milele, amjaalie umri mrefu, amruzuku ilmu na fahamu ili aweze kufanya tafiti nyingine zaidi, Insha-Allah. Tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.