Hotuba ya Mtume saww katika kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani -1
Hotuba ya Mtume saww katika kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani -1
0 Vote
231 View
Kama ambavyo mtukufu mtume jambo lake kuu ni kuweza kuuongoza umma kufikia katika malengo makubwa, basi swala zima la kutimiza ibada nzima ya funga kwa ukamilifu ni katika maswala yanayoambatana na kazi yake hiyo. Hivyo katika kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, aliweza kuwahutubia waumini kwa lengo la kuwapa maandalizi yatakayowawezesha kuufunga mwezi huu hali ya kuwa wana elimu tosha juu ya nini kifanyike na nini kisifanyike. Ifuatayo ni hotuba hiyo muhimu pamoja na tarijama yake: Amepokea Imamu Ally as kwamba siku moja mtukufu Mtume karibuni na mwezi wa Ramadhani aliwahutubia waumini na kuwaambia:
أَیهَا النَّاسُ إِنَّهُ قَدْ أَقْبَلَ إِلَیکمْ شَهْرُ اللَّهِ بِالْبَرَکةِ وَ الرَّحْمَةِ وَ الْمَغْفِرَة
"Enyi watu, kwa hakika mmejiwa na mwezi wa Mwenyezi Mungu kwa baraka na rehema na maghfirah (msamaha)..”شَهْرٌ هُوَ عِنْدَ اللَّهِ أَفْضَلُ الشُّهُورِ وَ أَیامُهُ أَفْضَلُ الْأَیامِ وَ لَیالِیهِ أَفْضَلُ اللَّیالِی وَ سَاعَاتُهُ أَفْضَلُ السَّاعَاتِ
" Ni mwezi ambao mbele ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko miezi mingine, na masiku yake ni bora kuliko masiku mengine, na usiku zake ni bora kuliko usiku nyingine, na hata masaa yake ni bora kuliko masaa ya miezi mingine..”وَ هُوَ شَهْرٌ دُعِیتُمْ فِیهِ إِلَی ضِیافَةِ اللَّهِ وَ جُعِلْتُمْ فِیهِ مِنْ أَهْلِ کرَامَةِ اللَّهِ
"Ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu amewaalika katika karamu yake, na amewakusanya katika wenye kustahiki kukirimiwa naye...”أَنْفَاسُکمْ فِیهِ تَسْبِیحٌ وَ نَوْمُکمْ فِیهِ عِبَادَةٌ وَ عَمَلُکمْ فِیهِ مَقْبُولٌ وَ دُعَاؤُکمْ فِیهِ مُسْتَجَابٌ
"Pumzi zenu katika masiku haya ni tasbihi, usingizi wenu ni ibada, matendo yenu ni yenye kukubaliwa, na dua zenu pia ni zenye kujibiwa....”فَاسْأَلُوا اللَّهَ رَبَّکمْ بِنِیاتٍ صَادِقَةٍ وَ قُلُوبٍ طَاهِرَةٍ أَنْ یوَفِّقَکمْ لِصِیامِهِ وَ تِلَاوَةِ کتَابِهِ
" Basi muombeni mola wenu kwa nia safi na nyoyo zilizotoharika, aweze kuwajaalia kuufunga na pia kusoma kitabu chake kitakatifu (Quran)...”فَإِنَّ الشَّقِی مَنْ حُرِمَ غُفْرَانَ اللَّهِ فِی هَذَا الشَّهْرِ الْعَظِیمِ
" Kwani mwovu kabisa ni yule ambaye atakosa kusamehewa katika mwezi huu mtukufu...”وَ اذْکرُوا بِجُوعِکمْ وَ عَطَشِکمْ فِیهِ جُوعَ یوْمِ الْقِیامَةِ وَ عَطَشَهُ
"Na kwa kupitia mwezi huu tumieni kiu na njaa yenu kukumbuka kiu na njaa ya siku ya kiyama...”وَ تَصَدَّقُوا عَلَی فُقَرَائِکمْ وَ مَسَاکینِکمْ
"Na toeni sadaka kwa ajili yenu na kwa ajili ya wasiojiweza kati yenu”وَ وَقِّرُوا کبَارَکمْ وَ ارْحَمُوا صِغَارَکمْ وَ صِلُوا أَرْحَامَکمْ
"Heshimuni wakubwa kwenu, hurumieni wadogo wenu, na ungeni udugu wenu..”وَ احفَظُوا ألسِنَتَکم، وغَضّوا عَمّا لایحِلّ النَّظرُ إلیه أبصارَکم، و عمّا لایحلّ الإستِماعُ إلیه أسماعَکم
" Hifadhini ndimi zenu, na inamisheni macho yenu kunako ambayo hayafai kuangalia, na zibeni masikio yenu kunako ambayo hayafai kuyasikiliza....”وَ تَحَنَّنُوا عَلَی أَیتَامِ النَّاسِ یتَحَنَّنُ عَلَی أَیتَامِکمْ
" waoneeni huruma mayatima wa watu ili na nyie muonewe huruma mayatima wenu..”تُوبُوا إِلَی اللَّهِ مِنْ ذُنُوبِکمْ
Tubieni kwa Mwenyezi Mungu kutokana na madhambi yenuوَ ارْفَعُوا إِلَیهِ أَیدِیکمْ بِالدُّعَاءِ فِی أَوْقَاتِ صَلَوَاتِکمْ فَإِنَّهَا أَفْضَلُ السَّاعَاتِ
" Na inueni kwake mikono yenu kwa ajili ya maombi katika nyakati za sala zenu, kwani nyakati hizo ni nyakati bora mno uliko nyingine zote...”یَنْظُرُ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ فِیهَا بِالرَّحْمَةِ إِلَی عِبَادِهِ، یُجِیبُهُمْ إِذَا نَاجَوْهُ وَ یُلَبِّیهِمْ إِذَا نَادَوْهُ وَ یَسْتَجِیبُ لَهُمْ إِذَا دَعَوْهُ
" Ni nyakati ambazo Mwenyezi Mungu huwaangalia waja wake kwa huruma, huwajibu pale wanapomuomba, huwaitikia wanapomuita, na huwapokelea pale wanapomuomba...”أَیهَا النَّاسُ إِنَّ أَنْفُسَکمْ مَرْهُونَةٌ بِأَعْمَالِکمْ فَفُكّوهَا بِاسْتِغْفَارِکمْ
" Enyi watu, hakika nafsi zenu zimewekewa rehani matendo yenu, basi zikomboeni kwa kuzidisha istighfar (msamaha)...”وَ ظُهُورُکمْ ثَقِیلَةٌ مِنْ أَوْزَارِکمْ فَخَفِّفُوا عَنْهَا بِطُولِ سُجُودِکمْ
" Na migongo yeni ni mizito kutokana na madhambi yenu, basi ifanyeni itoeni uzito huo kwa kurefusha sajda zenu...”وَ اعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ تَعَالَی ذِکرُهُ أَقْسَمَ بِعِزَّتِهِ أَنْ لایعَذِّبَ الْمُصَلِّینَ وَ السَّاجِدِینَ وَ أَنْ لایرَوِّعَهُمْ بِالنَّارِ یوْمَ یقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعالَمِینَ
" Na tambueni ya kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu ameweka kiapo ya kwamba hatowaadhibu wala kuwatishia moto wa jahanamu wenye kuswali na kusujudu sana siku ambayo viumbe vyote vitasimama mbele ya mola na mlezi wa walimwengu....”أَیهَا النَّاسُ مَنْ فَطَّرَ مِنْکمْ صَائِماً مُؤْمِناً فِی هَذَا الشَّهْرِ کانَ لَهُ بِذَلِک عِنْدَ اللَّهِ عَزَّ وَ جَلَّ عِتْقُ رَقَبَةٍ وَ مَغْفِرَةٌ لِمَا مَضَی مِنْ ذُنُوبِهِ
" Enyi watu! Mwenye kumfuturisha muumini aliyefunga katika mwezi huu basi atakuwa na malipo ya kumwacha huru mtumwa na pia atasamehewa dhambi zake zote zilizopita...”فَقِیلَ لَهُ یا رَسُولَ اللَّهِ لَیسَ کلُّنَا یقْدِرُ عَلَی ذَلِک فَقَالَ(ص) اِتَّقُوا النَّارَ وَ لَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ اتَّقُوا النَّارَ وَ لَوْ بِشَرْبَةٍ مِنْ مَاءٍ
Baada ya mtume kusema kauli hii watu walimuuliza na kumwambia " ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, sio kila mmoja wetu anaweza kufanya hivyo!”, mtume akajibu kwa kusema "Jiepusheni na moto hata kwa fundo moja la maji”. Kisha akaendelea kwa kusema:َیهَا النَّاسُ مَنْ حَسَّنَ مِنْکمْ فِی هَذَا الشَّهْرِ خُلُقَهُ کانَ لَهُ جَوَازاً عَلَی الصِّرَاطِ یوْمَ تَزِلُّ فِیهِ الْأَقْدَامُ
" Enyi watu! Mwenye kuwa na tabia nzuri katika mwezi huu atakuwa amejirahisishia kupita katika Sirat siku ya kiyama siku ambayo kuna nyoyo zitashindwa kupita....”وَ مَنْ خَفَّفَ فِی هَذَا الشَّهْرِ عَمَّا مَلَکتْ یمِینُهُ خَفَّفَ اللَّهُ عَلَیهِ حِسَابَهُ
" Na mwenye kupunguza majukumu kwa ambao anawamiliki basi Mwenyezi Mungu pia atampunguzia hesabu yake...”وَ مَنْ کفَّ فِیهِ شَرَّهُ کفف [کفَ] اللَّهُ عَنْهُ غَضَبَهُ یوْمَ یلْقَاهُ
" Na mwenye kuzuia shari yake kwa viumbe basi Mwenyezi Mungu pia atamkinga na hasira zake siku ambayo atakutana naye...”وَ مَنْ أَکرَمَ فِیهِ یتِیماً أَکرَمَهُ اللَّهُ یوْمَ یلْقَاهُ
" Na mwenye kumkirimu yatima basi Mwenyezi Mungu pia atamkirimu siku watakayokutana....”وَ مَنْ وَصَلَ فِیهِ رَحِمَهُ وَصَلَهُ اللَّهُ بِرَحْمَتِهِ یوْمَ یلْقَاهُ وَ مَنْ قَطَعَ فِیهِ رَحِمَهُ قَطَعَ اللَّهُ عَنْهُ رَحْمَتَهُ یوْمَ یلْقَاهُ
" Na mwenye kuunga udugu wake katika mwezi huu basi Mwenyezi Mungu atamuunganisha na rehema zake siku watakayokutana, na mwenye kukata udugu wake katika mwenzi huu basi Mwenyezi Mungu pia atamkatia rehema zake siku watakayokutana.....”