Bismillahi ni sehemu ya Qurani
Bismillahi ni sehemu ya Qurani
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2008
Publish location :
Dar es salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Bismillahi ni sehemu ya Qurani
Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: “al-Basmallah: Juz’iyyatuhaa wa ‘l-Jahrubihaa" Sisi tumekiita:“Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara.” “Kitabu hiki, “Bismillahi ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara." ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Sheikh Jafar Subhany. Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake. Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. BISMILLAH ni Aya? Hili ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote, wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.