Dua Iftitah
Dua Iftitah
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2016
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Dua Iftitah
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha dua (Kiarabu/Kingereza) kwa jina la A Manual of Ramadhan Devotion. Sisi tumekiita, Du’a za Mwezi wa Ramadhani. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa dua maarufu zinazosomwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Jambo bora kabisa ambalo muumini anaweza kuomba wakati wa mwezi huu ni maghfira na msamaha kutokana na dhambi zake zilizopita. Nyingi ya dua maalumu kwa mwezi wa Ramadhani ni za kuomba msamaha wa mzigo mkubwa wa dhambi ambao mtu ameubeba. Ramadhani ni nafasi nzuri sana aliyopewa yeye kufanya madhambi yake yafutwe na kujipatia cheo cha juu mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu. Kutokana na umuhimu wa dua hizi, tumeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa lengo letu lile lile lakuwahudumia ndugu zetu Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Ustadh Al Haji Hemedi Lubumba Selemani na Al Haji Ramadhani S. K. Shemahimbo, kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki katika kusahihisha na kukipitia hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwa wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa ibada na elimu katika dini.