Dua-za-Miezi-Mitatu
Dua-za-Miezi-Mitatu
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2013
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Dua-za-Miezi-Mitatu
Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni mkusanyiko wa dua mbalimbali ambazo zimetokana na Maasumina 14 (a.s) watokanao na nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Bwana Mtume amesema: “Dua ni silaha ya muumini,” hivyo ni kinga kwake pia. Utaona kwamba dua ni kitu muhimu sana kwa waumini; na hiki ndicho kilichomsukuma ndugu yetu Sayyid Aqyl kuzikusanya dua hizi ambazo ni muhimu sana na kuzitarjumi kwa lugha ya Kiswahili, lakini pia bila kuiacha lugha yake ya asili ambayo ni ya Kiarabu kwenda sambamba na Kiswahili. Na hili kwa hakika litamrahisishia msomaji wa Kiswahili hali kadhalika na msomaji wa Kiarabu kuzielewa vizuri dua hizi. Si mara ya kwanza kwa Sayyid Aqyl kuandika kitabu cha dua, kabla yake alitarjumi dua mashuhuri iitwayo, Dua Kumayl. Tunamshukuru sana kwa juhudi zake hizi za kuwahudumia waumini wenzake. Tunamuomba Allah ampe wasaa zaidi katika juhudi zake hizi, na ampe afya njema ili aweze kutekeleza wajibu huu. Taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa makubwa kwao. Tunawashuku wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera pia. Amin!