Historia na Sira za Viongozi Waongofu Sehemu ya Kwanza

Historia na Sira za Viongozi Waongofu Sehemu ya Kwanza

Historia na Sira za Viongozi Waongofu Sehemu ya Kwanza

Interpreter :

Hemedi Lubumba

Publication year :

2010

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Historia na Sira za Viongozi Waongofu Sehemu ya Kwanza

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Tarikh wa Sirati ‘l-Qadati ‘l- Hudaah. Sisi tumekiita,Historia na Sira za Viongozi Waongofu. Kitabu hiki ni matokea ya kazi ya kielimu iliyofanywa na wanavyuoni wa Kiislamu waliomo kwenye Jopo la Waandishi wa Vtabu vya Kiada katika Taasisi ya Kimataifa ya Hawza na Madrasa. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.