JANNAT na JAHANNAM ( Peponi na Motoni )

JANNAT na JAHANNAM ( Peponi na Motoni )

JANNAT na JAHANNAM ( Peponi na Motoni )

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

JANNAT na JAHANNAM ( Peponi na Motoni )

Ingawaje Qur’an Tukufu inatujulisha vya kutosha kuhusu Jannat (Peponi ) na Jahannam ( Motoni ), vile vile tunapata habari zaidi kutoka Ahadith Qudsi zilizoletwa na Malaika Jibraili a.s. kwa Mtume Muhammad s.a.w.w. ambaye ananakiliwa na Imam Ali a.s. na Maimamu Kumi na moja a.s. waliobakia. Mtume s.a.w.w. wakati wa Me’raj aliweza kuona na kutembea Jannah au Peponi, kula matunda ndani mwake na kuangalia yale yaliyokuwamo. Vile vile alitembelea Jahannam au Motoni ambamo aliweza kuwaona wale kujionea vile wahalifu walivyokuwa wakiadhibiwa kwa madhambi yao. Al Tirmidhi na Abu Daud wananakili Ahadith Qudsi ifuatayo kutoka kwa Mtume Muhammad s.a.w.w.: Allah swt alipoumba Jannat na Jahannam, alimtuma Malaika Jibraili a.s. kwenda Jannat, akisema, “Angalia ndani mwake kile nilichokiwatengenezea wakazi wa humo.” Malaika Jibraili a.s. alikwenda akaangalia vizuri na kwa makini, na aliporudi kwa Allah swt alisema, “Kwa utukufu wako Naapa kuwa hakuna atakayeisikia illa atatamani kuingia humo.”