Khazina ya Mu’mini
Khazina ya Mu’mini
Publisher :
Publication year :
2007
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
(0 Kura)
(0 Kura)
Khazina ya Mu’mini
Kijitabu hiki kina dua ambazo husomwa kila baada ya swala tano zinazoswaliwa kila siku. Kadhalika kuna dua makhsusi zinazosomwa kwa siku makhsusi, kila siku na dua yake. Dua hizi ni mashuhuri sana na tumezipokea kutoka kwa Imam Aly ibnul Hussein Zaynal Abideen (AS). Pamoja na haya kuna Ziarah za watakatifu 14 ambazo pia zimepangiwa siku zake za kusoma. Inasemwa kuwa dua haisomwi kama kasuku bali inatakiwa iombwe kwa kuelewa unaomba nini na kwa unyenyekevu na kwa kuwepo kwa fahamu zetu katika kitendo hicho cha kuomba, isiwe mtu anasoma dua lakini anafikiria mechi ya mpira. Maimamu (AS) pia wametueleza utaratibu wa kuomba dua. Nayo ni kuwa ni vizuru uwe na udhu, utamke Bismillah kabla na pia umsalie Mtume (SAWW) na kizazi chake kabla ya kuanza na mwisho wa dua. Kwani tunambiwa kwa kuwa Allah ataikubali swala ya Mtume (SAWW) mwanzoni na mwishoni basi bila shaka atakuibali na dua yenyewe iliyopo katikati, kwani Mungu sio bakhili. Ni mategemeo msomaji utanufaika kwa kusoma dua hizo na pia ukazileewa zinasemaje kwa kusoma tarjuma yake kwa kiswahili