Kupunguza Swala Safarini
Kupunguza Swala Safarini
Author :
Interpreter :
Publish number :
Toleo la kwanza
Publish location :
Dar-es-Salaam, Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Kupunguza Swala Safarini
Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "" Sisi tumekiita: "Kufungua safarini." Kitabu hiki, "Kufungua safarini" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Sheikh Jafar Subhany. Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake. Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. Kufungua safarini ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.