KUSOMA SURA ZENYE SIJDA ZA WAJIBU KATIKA SALA
KUSOMA SURA ZENYE SIJDA ZA WAJIBU KATIKA SALA
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2010
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
KUSOMA SURA ZENYE SIJDA ZA WAJIBU KATIKA SALA
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Qira’atu ‘l-’Aza’im Fi ‘s-Swalah. Sisi tumekiita, Kusoma Sura zenye Sijda za Wajibu katika Sala. Kitabu hiki kimeshughulikia suala la usomaji wa sura ambazo ndani yake kuna aya za “sijda wajibu.” Kuna tofauti kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili, na halikadhalika kuna tofauti ndani ya madhehebu za Sunni zenyewe. Wanazouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu, wamehitilafiana katika hukumu ndogondogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanazuoni kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zogo lisilo na maana. Mambo ambayo wanazuoni wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo] hayana nafasi tena katika akili za watu. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukiftarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.