Drawer trigger

Qur’ani Yatoa Changamoto

Qur’ani Yatoa Changamoto

Qur’ani Yatoa Changamoto

Mchapishaji :

AL-ITRAH FOUNDATION

Mwaka wa uchapishaji :

2008

Eneo la uchapishaji :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Qur’ani Yatoa Changamoto

Kitabu ulicho nacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la al-Qur’an Yatahaddaa kilichoandikwa na Marehemu Ayatullah Sayyid Muhammad Husaini Shirazi. Sisi tumekiita Qur’ani Yatoa Changamoto.
Kila Mtume au Nabii alikuja na muujiza wake na alipoondoka muujiza wake huo ulikoma kuwepo pia. Kwa mfano, Nabii Ibrahim (a.s.) muujiza wake mkubwa ilikuwa kwamba alipotupwa kwenye tanuri ya moto kwa nia ya kumteketeza, moto ule ukawa baridi juu yake. Fimbo ya Nabii Musa (a.s.) ilikuwa ikitenda miujiza mingi - iliweza kugeuka kuwa joka kubwa la kutisha, ilipasua bahari na kutoa njia kwa Wana wa Israil kuweza kuvuka bahari kwa salama bila ya kutumia chombo, n.k. Nabii Isa (a.s.) alikuwa akiponya vipofu, wakoma na hata kufufua wafu
kwa idhini ya Allah (Mwenye kuhuisha, Aliye Hai). Lakini Mitume hao walipoondoka na miujiza yao pia ikatoweka pamoja nao. Mtume Muhammad (s.a.w.) ambaye ni mwisho wa Mitume, naye kaja na miujiza mingi, lakini ulio mkubwa kabisa ni Qur’ani Tukufu ambayo ni muujiza ambao umebakia baada ya kuondoka kwake. Qur’ani ni muujiza kwa sababu inakwenda na wakati na inakubalika katika kila karne na kizazi. Kwa mfano, wanasayansi wa leo wanagundua mambo ambayo yalikuwa yameshaelezwa na Qur’am Tukufu zaidi ya karne 14 zilizopita, na hapana shaka, wataendelea kila karne kugundua mambo ambayo tayari maelezo yake yamo katika
Qur’ani. Hii ndio maana tunaposema kwamba Qur’ani ni muujiza uliohai na utabakia kuwa hai mpaka mwisho wa duma. Qur’ani yenyewe inatoa changamoto kwa usahihi wake kwa wale wote wanaoitilia shaka, wakiwemo majini na wanadamu, kwamba watoe mfano wa hii Qur’ani. Hii ni karne ya 15 tangu Qur’ani Tukufu iteremshwe kutoka mbinguni, na hakutokea jini wala binadamu yeyote aliyeweza kutoa mfano wake.